NOTE: MTANDAO HUU KUTOKEA NAIROBI HAUMILIKI SIMULIZI ZA AINA YOYOTE BALI INAZIKUSANYA KUTOKA KWENYE VYANZO MBALI MBALI KAMA FACEBOOK, WHATSAPP, NA YOUTUBE


Ilipoishia..
“Abubakar Saireee, kuna mgeni wakooo” ilikuwa ni sauti ya askari ikinishtua kutoka katikati ya dimbwi kubwa la mawazo. Nikasimama na kumfuata askari yule..
Endelea..
Safari yangu na askari yule ikatuchukua mpaka kwenye chumba kidogo ambamo niliingia nikamkuta bwana Filbert Tago ambaye alikuwa ni hakimu na bwana ambaye alipotelewa na binti yake akiwa ananisubiri. Alikuwa amekaa juu ya kiti kimojawapo katika chumba kile chenye viti viwili na meza.
Nikaenda na kukaa kwenye kiti kile kingine tukawa tukitizamana. “Nataka uniambie ukweli juu ya jambo hili” alisema bwana yule kufungulia maongezi. Nilibaki kimya nikiwaza, kama huyu bwana amenifuata mpaka huku basi ana nia ya kunisaidia kwa maana sio jambo la kawaida hakimu kumtembelea mshtakiwa, sidhani hata kama inaruhusiwa kisheria “sii sio kesi ndogo, iwapo utashindwa utafungwa miaka mingi sana.
Na iko wazi kuwa utashindwa maana kuna ushahidi wa kutosha kuwa ulitoroka” aliongeza bwana yule nami nikamueleza kuwa nilitoroka kichawi, jambo ambalo aliliamini mara moja kinyume na mategemeo yangu.
“Sikia, mimi najua kuwa unayo mbinu ya kumpata mkeo. Unaonaje kama nitakusaidia ili na wewe unisaidie kumkumbuka binti yangu wakati wa kumsaidia mkeo?”. Hii ni fursa pekee ya kuharakisha zoezi la kumpata mke wangu ambaye anakabiliwa na mambo mawili mbele yake ambayo mpaka sasa sijui lipi litampata au limekwishampata, kuna uwezekano wa kuolewa Magugi lakini pia nilielezwa juu ya kufa kwake baada ya kijifungua.
“Sina muda wa kutosha hapa” niligutushwa na sauti ya bwana Tago kutoka kwenye mawazo ambamo nilipotelea humo. “Sawa bwana, tushirikiane katika hili” nilijibu kisha kumuelezea bwana yule kila kitu juu ya mipango yangu na Mnaro naye akaahidi kunisaidia ila akinitaka kuhakikisha kuwa namrudisha binti yake kutoka Muifufu, tukakubaliana ba mimi kurudi mahabusu nikiwa na matumaini mapya.
Ile siku ikaisha mahabusu ndani ya jela ile.
“Huyu mwingine analala kama vile yuko kwake, aisee amkaaa” nilisikia mtu akizungumza huku akinitikisa kuniamsha. Nikaamka na kukutana na bwana mmoja mkubwa sana wa umbo. “Twende ukafanye kazi kumekucha” alisema bwana yule akinikabidhi fagio nami nikatii haraka kwakuwa sikutaka kujenga chuki ndani ya mahabusu ile kuhofia kuwa na maisha magumu zaidi.
Nikaongozana na bwana yule hadi kwenye eneo la vyoo akanitaka kufanya usafi humo. Nilichungilia ndani ya vyoo vile na kwakweli hali ilikuwa ikitisha. Kulikuwa ni kuchafu mno, sidhani kama vyoo vile viliwahi kusafishwa. Kinyesi kilikuwa juu juu kikielea juu ya maji ambayo sikujua yametoka wapi ndani ya vyoo vile.
Nikawaza kubishia kazi ile, ila nilipomuangalia bwana yule ambaye inaelekea alikuwa kiongozi ndani ya mahabusu nilimuona fika kuwa amejiandaa kukabiliana nami iwapo nitakataa kazi ile.
Nikaamua kuwa mpole, nikainama na kuanza kukunja suruali yangu ambayo kama ningeingia bila kuikunja bila shaka ingecheza na kinyesi.
Wakati nikiendelea kukuja suruali yangu mara nikasikia sauti ikiita “Jafariii, namuomba huyo jamaa” nikageuka na kumuona askari wa magereza akimuagiza bwana yule.
“Kamsikilize afande kwanza ila mkimalizana tu urudi haraka, kazi inakungoja hii” alisema bwana yule nami nikaondoka na kumfuata askari yule tukaongozana “una bahati mbaya sana bwana” alisema askari yule nikashtuka na kujiuliza nini kilikuwa kinakwenda kunipata tena “yani umekuja jana tu leo unaondoka? Bado hujajifunza maisha wewe, ilipaswa ukae angalau miezi miwili bwana” alisema askari yule kiutani huku akicheka.
Nivuta pumzi nyingi nikaiachia yote. Nikamshukuru mungu kimoyomoyo kwa wema ambao amenitendeat.
Tuaenda mpaka mapokezi ya gereza lile ambapo nilielezwa kuwa wamepokea hati ya dhamana kutoka mahakamani hivyo natakiwa kwenda nyumbani lakini nihudhurie mahakamani tarehe ambayo ilipangwa kesi yetu isikilizwe tena.
Nikapewa vitu vyangu ambavyo walinihifadhia na kwenda nyumbani.
Nilifika nyumbani na kukimbilia bafuni kabla ya chochote, mwili wangu nilikuwa nauona kama wa ambae alilala jalalani kutokana na mazingira machafu ya ndani ya magereza.
Baada ya kuoga nikakaa nikijiuliza nawezaje kumpata Mnaro, nilikuwa nikimuhitaji sana lakini sikuwa nikijua namna ya kufika kwake ingawa nimeenda mara kadhaa, hii ni kutokana na yeye kuwa ananichukua kiuchawi kwenda huko kila wakati ambao alitaka twende, hivyo sikuijua njia ya kwenda huko.
“Hii ni mara ya mwisho kukufuata, wakati mwingine utakuwa unakuja mwenyewe” niliikumbuka kauli hii ya Mnaro nikajikuta nimetoa msonyo mkubwa sana.. alitegemea nitakuwa naenda mwenyewe ikiwa sipajui? Niliwaza nikijilaza kitandani na usingizi haukuwa na hiana, ukanipokea vizuri nikalala fofofo.
Niliposhituka ilikuwa ni majira ya saa saba usiku lakini Mnaro hakuwa amekuja. Nikaamua kutoka na kwenda kufanyia mazoezi ambacho alikwishanifundisha. Nikamchukua yule paka, ambaye sasa nilikuwa nimemuweka kwenye banda kubwa nyuma ya nyumba yangu ambalo lilitengenezwa kwaajili ya kufugia kuku lakini halikuwa likifanya kazi hiyo kwa wakati huu.
Nikaingia mitaani nikiwa namuendesha paka yule, nilikuwa nimejua kila kitu kuhusu namna ya kumuendesha paka yule na nilikuwa nikifurahia sana utendaji wake hasa uwezo wa kwenda umbali mrefu ndani ya muda mfupi tu.
Nikawa nimeenda mbali zaidi ambapo hata sikuwahi kufika kabla nikaona kwa mbali nyuma yangu kuna mtu anakuja uelekeo niliopo akiendesha mnyama ambaye kwa umbali ule sikuweza kumtambua. Nikaamua kujificha nyuma ya mti mkubwa wa mbuyu ambao niliuona mbele yangu ili kumpisha mtu huyo apite kwamaana sikujua kama alikuwa ni mwema kwangu ama laah!..
Nikiwa nachungulia nyuma ya mbuyu ule niliona mtu yule akija juu ya mnyama ambaye sasa niligundua kuwa alikuwa ni paka kama huyu wakwangu akija mpaka mbele ya mbuyu ule kisha akasimama, tukawa tumetenganishwa na mbuyu tu, mimi nikiwa nyuma na yeye akiwa mbele.
Nikapatwa na uoga kidogo nikijiuliza mtu yule alikuwa na lengo gani kusimama pale? Au atakuwa ameniona? “Umejificha lakini uoga unakuumbua, unapumua kwanguvu mpaka nakusikia” ilisikika ikisema sauti ya mtu yule nyuma ya mbuyu nikagundua mara moja kuwa alikuwa MNARO.
Nikatoka nyuma nyumauyu mbuyuanikiwarahafurahao sikujusikujuakkwa maana nilkwawa nikasirishwailitoka mnharamno na mwenendo wa Mnaro na kutamani angalau ningekuwa na uwezo wa kumchapa hata kibao tutakapo onana
“Ulikuwa wapi siku zote hizi aisee? Nimekusubiri sanaaa” nilisema huku nikishindwa kuzuia tabasamu la furaha.. “mimi ndo nikuulize wewe ulikua wapi? Ulikuwa unaningoja kwani tulikubaliana kuwa nitakuja?” Aliuliza Mnaro nami nikabaki kumshangaa kwa maana wakati wote aluokua anaingia chumbani kwangu bila hodi kama kwake hatukuwa tumekubaliana kama atakuja.
“Nadhani mara ya mwisho kukufuata nilikwambia waziwazi kuwa ilikuwa ni mara ya mwisho kukufuata na baada ya hapo ungekuwa unakuja mwenyewe” aliongeza maelezo Mnaro. “Sasa nawezaje kuja ikiwa sipajui pa kukupata?” Niliuliza swali ambalo nililiona ni la msingi lakini Mnaro akanitizama kama ambaye naongea ujinga “leo ndo unauliza hilo swali? Nadhani ulipaswa kuuliza wakati nakwambia kuwa sitokufuata tena. Tatizo lako unaishi kwaajili ya leo tu wala hujisumbui kuiwaza kesho” alisema Mnaro nami nikajiona kweli nilikuwa, nikaamua kuwa mpole.
“Nilipatwa na matatizo bwana” niliamua kubadili mada baada ya kuona lawama zangu zinanirudia mwenyewe. “Ninajua kila ambacho kilikupata. Najua ulitegemea nikusaidie lakini sipo kwaajili ya kukusafisha kila ukijichafua, huko ni kukulemaza. Kumbuka Muifufu hautomwenda na mimi” alisema Mnaro nami nikabaki bila hoja.
“Kwakuwa tumekutana nadhani tugange yaliyopo na yajayo, bora tuanze mafunzo” nilisema kumwambia Mnaro ambaye alitabasamu na kisha akajibu “sielewi kwanini huoni kama hapa tunajifunza, maisha yote ambayo unaishi toka nianze kukufundisha ni mafunzo sio kushika matunguri tu” alisema Mnaro ambaye niliona kama leo ameamua kunionesha ni jinsi gani mimi sijui kufikiria.
“Umejifunza mambo mengi sana ndani ya muda mfupi, tena kwa vitendo. Kapumzike uyafanyie kazi hayo kisha tukutane keshokutwa kwaajili ya kumalizia mafunzo” alisema Mnaro ambaye nilianza kumuona kuwa amekwishazoea hali ya mpenzi wake kuishi Muifufu huku yeye akiwa huku.
Anaachaje kuzoea ndani ya miaka yote ambayo amekuwa mbali na huyo mpenzi wake, niliwaza. Ambacho hakielewi ni kuwa mimi siko tayari kuandamwa na tatizo hili kwa muda mrefu kiasi hicho.
“Tukutane keshokutwa” alisema Mnaro akianza kuonda.. “sasa nitakupataje hiyo kesho kutwa?” Niliuliza Mnaro akaniangalia akitabasamu “unaona bwana, vitendo vinafunza zaidi ya maneno. Sasa unajua kuiwazia hata keshokutwa” alisema kisha akatoa kakioo kadogo kutoka kwenye ule mkoba wake wa ngozi na kunikabidhi.
“Sema na hicho kioo ukinihitaji nacho kitanileta” alisema Mnaro na kupotelea mbali na yule paka wake akiniacha nikikitalii kioo kile ambacho kilikuwa chakavu kikiwa kimefungwa na mipira kukizunguka.
Nikaondoka kuelekea nyumbani kwa usafiri wa paka yule ambaye hakuchukua muda kinifikisha mtaani kwetu lakini nilisita nikaangalia kwa mbali na kuona nnje ya nyumba yangu kukiwa na kikundi cha watu wakiwa busy kufanya shughuli ambazo sikuzielewa.
Nika shuka juu ya paka yule huku nikimnong`oneza kuwa nimkute hapo ninapomuacha.
Nikasogea karibu na nyumbani kwa mwendo wa kuchuchumaa kukwepa watu wale wasinione. Nikafika karibu kabisa mpaka nikaweza kuwaona watu wale.
Nimgundua mmoj wa watu wale ambaye ndiye aliyeonekana kuongoza kundi lile, alikuwa ni mwanamke yule ambaye alikuja kuniwangia nikamkimbiza na kukimbilia kwa wachawi wenzake.
ITAENDELEA..

Facebook Comments

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here