NOTE: MTANDAO HUU KUTOKEA NAIROBI HAUMILIKI SIMULIZI ZA AINA YOYOTE BALI INAZIKUSANYA KUTOKA KWENYE VYANZO MBALI MBALI KAMA FACEBOOK, WHATSAPP, NA YOUTUBE

ILIPOISHIA
kweli hakuamini msalaba uliokua mbele yake ulioonesha jina la Jesca Abel huku na picha yake ikiwepo kwa juu yake, hapo ndipo alihisi nguvu zinamuishia mwilini mwake.
“Hapana Jesca sio kweli, sio kweli”
Alijikuta akilia machozi na kusogea karibu mpaka kwenye kaburi la mpenzi wake huku akikumbuka vitu vingi vilivyopita katika maisha yao…..
SONGA NAYO.
Dokta Emmanuel Kway yupo makaburi ya kinondoni analia na kuomboleza siku mbili mfululizo,bado aliona mambo yanayotokea hayakuwa halisi bali yupo ndotoni na muda mfupi angeshtuka na kumuona Jesca Abel Mpenzi wake yupo hai wanafurahi na kuendeleza ndoto zao.
Ni kweli mwanamke huyo hakustaili kufa mapema kiasi hiko.Fikra zake zilirudi nyuma haraka haraka na kukumbuka mambo yaliyotokea kanisani alivyokua akifunga ndoa na Doreen Buchanan mtoto wa Raisi wa Rwanda kisha Jesca Abel kutokea, aliamini kuwa halikua kosa lake sababu alidhani amekufa.
Hapo ndipo alipoamua kughairi kufunga ndoa na kuanza kumfukuzia mwanamke huyo ambaye aliyedhani amekufa kwenye ajali mbaya ya Meli ya MV BUKOBA iliyozama na kuchukua roho za mamia na maelfu ya watu , kilichomchanganya tena ni kushuhudia ajali mbaya aliyoishuhudia kwa macho yake kisha baadaye kuambiwa Jesca Abel amefariki Dunia.
Alijiona ni muuaji sababu bila yeye wenda Jesca angekuwa hai. Siku mbili nzima alikua akikesha makaburini akiomba msamaha huku akitoa machozi kama mtoto,Moyo ulimuuma sana.
“jesca,naamini unanisikia huko Ulipo, naomba unisamehe Jesca wa…ngu ki ukweli nilidhani haupo tena duniani ndi..io maana nikachukua jukumu la kuoa Mwanamke mwingine ni..kiamini kuwa nitakusahau”
Dokta Kway aliongea huku akilia kwa kwikwi akibubujikwa na machozi, haikuwa kazi rahisi kumsahau mwanamke huyo ndani ya mtima wake hata kidogo!.
Ni kweli walipitia mengi sana katika maisha yao, wenda bila Jesca Abel asingekua daktari bingwa wala asingesoma,wazazi wake walikua ni maskini fukara wa kutupa walishindwa kumuendeleza kimasomo, lakini Mwanamke ambaye amelala ndani ya kaburi aliweza kumsaidia kwa kila kitu ivyo ndivyo ilivyokuwa.
***
Doreen Buchanan alishindwa kuelewa ni kitu gani kili mpata Mume wake mtarajiwa Dokta Kway,kitendo cha kufanya mipango ya kufoji kifo cha Jesca Abel yeye na Baba yake ambaye aliyekua kikwazo cha ndoa yake kukamilka na kuhiaribu alipotokea tu kanisani, aliamini mambo yangeenda vizuri na ndoa kufungwa haraka haraka ili waishi na mwanaume huyo aliyempenda sana na wajenge familia.
Asubuhi alivyoshtuka kitandani alipapasa mkono wake upande wa kushoto alipozoea kulala mchumba wake na kushtuka baada ya kugundua Dokta Kway hayupo ilikua ni asubuhi sana!.
“Honey”
Aliita Doreen huku akikaa kitako kitandani.
“Honey”
Alisimama kitandani huku akiwa amejifunika na shuka mpaka bafuni lakini bado hakumuona mchumba wake.
Hapo ndipo alipokumbuka kuwa ni lazima atakuwa kinondoni makaburini, alijimwagia maji haraka haraka na kuvaa nguo kisha kuingia ndani ya lift iliyompeleka mpaka chini na breki ya kwanza alifika mapokezi!.
“Mume wangu ulimuona leo hapa?”
“ndio alitoka asubuhi sana”
“hakusema anaelekea wapi?”
“hapana hakusema”
“sawa Ahsante,Muheshimiwa akiniulizia mwambie nimetoka”
Doreen aliacha ujumbe huo kisha kuingia milango ya nyuma ya gari na dereva kuondosha gari baada ya kuambiwa kuwa waelekee kinondoni makaburini.
Ni kweli baada ya kufika walimuona Kway analia sana amelala juu ya kaburi la Jesca Abel huku akilia machozi, bado alikua mwenye simanzi ilikua ni vigumu kumsahau mwanamke huyo, hata Doreen alishaanza kuingiwa na mashaka.
“Jesca nimekuja te…na nimeshindwa kukuacha peke yako ulale mwenyewe hapa,leo tulale wote mpenzi wangu”
Hayo ndiyo maneno aliyokua anaongea Dokta Kway akiyarudia tena,
Doreen alishtuka sana kusikia habari hiyo alimsogelea karibu kisha kumkumbatia kwa nyuma.
“Honey,unamkufuru Mungu usiseme ivyo,inakubidi usahau ili tufanye mambo mengine”
“Siwezi kumsahau, Jesca nimeongea naye jana usiku aliniambia anasikia baridi nije kulala naye”
“hapana mpenzi punguza mawazo ameshakufa tayari, usiwe ivyo mume wangu”
“Jana nimeongea naye kusema ukweli, tumeongea mengi sana”
“itakua uliota Darling,twende nyumbani ukale basi”
Doreen alijaribu Kumsihii mchumba wake,ilibidi kama mwanamke amfanye asahau amuoneshe kila aina ya upendo ili aweze kumsahau Jesca Abel.
Haikuwa kazi rahisi kama alivyo dhani kila kukicha jina Jesca ndilo lilitajwa wakati mwingine hata katikati ya usiku Dokta Kway akishtuka humtaja Jesca. jambo hilo lilizidi kumuumiza sana Doreen akilini mwake.
“Honey unaenda wapi?”
“Jesca ananiita”
Ilikua ni katikati ya usiku wa saa nane, ni kitendo cha Dokta Kway kuzinduka usingizini, kweli alimaanisha na kile anachokiongea, alivaa suruali yake na kutoka nje huku Doreen akiwa nyuma yake anamfuata akimuita. Aliwasha gari mpaka kinondoni makaburini bila kuogopa kitu chochote kile, ni kweli alivyofika kwenye kaburi la Jesca alianza kulia tena kama mtoto mdogo akiongea maneno yasiyoeleweka,ili kua ni picha ya kutisha.
Doreen alishaanza kuingiwa na wasiwasi wenda mchumba wake akili zake zimeanza kumruka sababu halikua jambo la kawaida,
nayeye aliingia kwenye gari usiku huo huo mpaka makaburini na kushtuka baada ya kumuona Dokta Kway anaongea peke yake!.
“nimekuja Mpenzi wangu Jesca usilie bado nakupenda tu,nitaendelea kukupenda sana,unaona nimekufuata mpaka huku,nakupenda kweli!”
Dalili zilionesha kuwa atakuwa mwendawazimu kama jambo hilo Doreen atalifumbia macho, ilibidi wakae wote makaburini mpaka kunakucha huku Dokta kway akiongea na kutaja jina Jesca, kitendo cha kutoka hapo ilibidi ampigie simu mwanasaikolojia dokta Frank Masai aliyebobea na kucheza na akili za binadamu,walipanga wakutane siku hiyo hiyo jioni yake.
Alishaamini tayari Dokta Kway alimeathirika kisaikolojia na ndio ushauri aliopewa kutoka kwa marafiki zake la sivyo Kway atakuwa mwenda wazimu kabisa.
“Nafikiri ndiye Dokta Frank Masai niliyekua naongea naye muda mfupi uliopita?”
Aliuliza Doreen Buchanan baada ya kukutana kwa mara ya kwanza na dokta huyo aliyepewa namba zake kisha kuamua kumtafuta kwa njia ya simu na kukutana naye Rose Garden ili aweze kumuelezea tatizo la Mchumba wake Kway.
“Ndiye Mimi naitwa Dokta Frank Masai, ni mwanasaikolojia,nakusikiliza dada angu”
Hapo ndipo Doreen alipoanza kumuelezea mwanasaikolojia huyo kila kitu kuanzia harusi ilivyoharibika alipotokea Jesca Abel mpaka kifo cha mwanamke huyo kilivyotokea na kitendo cha Dokta Kway kukesha makaburini akiongea peke yake.
Habari izo zilimfanya Frank Masai atingishe kichwa chake.
“Ulisema kuwa Jesca Abel alifariki?”
“Ndio amefariki kwenye hiyo ajali”
“Na ndiye huyo aliyefanya harusi yako iharibike baada ya kutokea?”
“Ndio”
“Kabla ya harusi yako kipindi mlivyokua na mahusiano na huyo Kway alishawahi kukwambia habari za Jesca?”
“Well, kuna siku tulikua chumbani kipindi tupo India masomoni,kuna picha niliona kwenye wallet yake ya huyo Jesca, nilipomuuliza ni nani akaniambia atanielezea ukweli tukimaliza mitihani lakini mpaka hapo nikasahau tena kumuuliza na ndiyo huyo dada alitokea kwenye harusi yetu ikaharibika”
“Ina maana kivyovyote walikua wana mahusiano?”
“Nilivyosikia lakini, kuwa alidhani amefariki kwenye ajali ya MV Bukoba sijui,na kudhani alikufa”
“Nani alikupa izo habari?”
“Wazazi wa huyu Mume wangu Baba Emma na Mama Emma!”
“okay! Inabidi twende naye taratibu, kwa harakaharaka mume wako ana Brain transshipment bado anadhani Jesca yupo hai, ni tatizo dogo kwangu inabidi twende naye taratibu sana, jesca angekuwa hai ndiyo hali yake ingerudi, kwa sasa hivi inabidi tufanye mambo taratibu”
“Nitashukuru sana, naomba hata sasa hivi kama una uwezo tafadhali”
“Sawa nitafanya hiyo kazi, yupo wapi?”
“Twende nitakupeleka”
Hapo hapo waliingia ndani ya magari yao na kuanza kuongozana mpaka Kilimanjaro hotel posta, lakini kilichowashangaza hawakumkuta Dokta Kway.
Doreen hakua na haja ya kuumiza kichwa chake alijua tu ni lazima atakua makaburi ya kinondoni na ndo hapo walipoanza safari mpaka makaburi ya kinondoni.
Wote walipigwa na butwaa walishtuka baada ya kumuona amelala juu ya kaburi amejifunika na shuka, halikua jambo la kawaida kwa binadamu mwenye akili timamu kufanya kitu kama hiko hata kama alifiwa na Mama yake mzazi.Dalili zilionesha wazi wazi kuwa Dokta Kway amerukwa na akili zake kichwani.
“Honey”
Aliita Doreen huku akimtingisha
“Jesca Jesca jescaaaa My Loveee,”
Alikurupuka Kway na kumkumbatia Doreen Buchanan huku akilia tena,
“Jesca ulikua wapi, nilikua nakutafuta sana mpenzi wangu,nimekaa hapa muda sana mke wangu vipi unaweza kutembea sasa, daktari keshakupatia matibabu?”
Doreen aliangua kilio hapo hapo sababu dalili zilionesha kuwa Dokta Kway amechanganyikiwa amerukwa na akili tayari, amekuwa mwendawazimu.
“Mhh.. lakini wewe sio Jesca, namtaka jesca wangu yuko wapi jamani, yuko wapi yuko wapiiiii Jesca. Mv Bukoba ajali. amekwenda wapi Mwanza au wapi, mpigie simu basi aje hapa mwambie namsubiri ubungo Mataa,twende Moshi, Marangu na Tarakea mpaka Himo”
Maneno hayo tu yalidhihirisha kuwa teyari Kway amekuwa mwendawazimu kabisa, Frank Masai mwanasaikolojia nayeye alikuwa pembeni amesimama, alishalijua hilo na kutoelewa ni kitu gani akifanye, alishachelewa tayari, akili zake teyari zilikua zimeharibika kwa ujumla, alianza kutembea huku na kule  huku akilitaja jina Jesca kisha kukimbia na kutokomea mbali na kumfanya Doreen alie machozi sababu mpaka usiku unaingia hakuweza kumuona Mchumba Wake Dokta Emmanuel Kway ni wapi alipoelekea……..
ITAENDELEA..


Facebook Comments

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here