Historia ya Kanisa Katoliki iliandikwa na kuhifadhiwa, historia iliyobeba mengi yenye kufurahisha, kusikitisha, kuchekesha, kuogofya, kufundisha na hata kuleta aibu kubwa kiasi mengine yamefichwa na kuwa siri, lakini sikuzote siri siyo ya watu wawili.

Je ni kweli kwamba mnamo karne ya 9 mwaka 847 alikuwepo Papa Joan… mwanamke aliyejifanya mwanaume na kuhudumu kama Papa wa Kanisa Katoliki kwa muda wa miaka 2 bila kujulikana jinsia yake?

Kwenye makabrasha ya historia ya kanisa katoliki(Roman Catholic Archives) kuna kila aina ya ushahidi kuwa alipata kuwepo Papa Joan, hata katika sanaa za michoro ya Rumi na vitabu mbali mbali, lakini Kanisa Katoliki linakanusha habari hizi.

pope-joan-statue-in-rome-jpg.805198Mary Marlone ambaye aliwahi kuwa mtawa(Sister) wa kanisa katoliki anasema kuwa hata yeye aliwahi kusoma uwepo wa Papa Joan na anaamini kabisa kuwa ni kweli Joan aliwahi kuwa Papa, tena mwanamke.

Mwingine ni Donna Cross, mwandishi wa vitabu ambaye alitumia muda wa miaka saba kujifunza mambo ya uandishi wa kale, anasema kuwa kuna maandishi ya kihistoria zaidi ya 500 huko Italia yanayozungumzia uwepo wa Papa mwanamke alijulikana kama Joan Anglicus.

Mary Marlone ambaye aliwahi kuwa mtawa(Sister) wa kanisa katoliki anasema kuwa hata yeye aliwahi kusoma uwepo wa Papa Joan na anaamini kabisa kuwa ni kweli Joan aliwahi kuwa Papa, tena mwanamke.

Mwingine ni Donna Cross, mwandishi wa vitabu ambaye alitumia muda wa miaka saba kujifunza mambo ya uandishi wa kale, anasema kuwa kuna maandishi ya kihistoria zaidi ya 500 huko Italia yanayozungumzia uwepo wa Papa mwanamke alijulikana kama Joan Anglicus.

Ushahidi katika kazi za sanaa za Rumi


Ukitembelea nchi ya Italia, jiji la Roma na kuwauliza wenyeji kuhusu Pope Joan, watakuonesha michoro ya sanaa, maandishi, na mashairi ya zamani yenye kumtaja Pope Joan. Mshahiri nguli wa zamani wa Rumi aliyeitwa Giovanni Boccaccio ambaye anajulikana sana kwa shairi lake maarufu linaloitwa “The Decameron,” pia aliandika kitabu kinachoitwa “The 100 Famous Women” na katika orodha hiyo ya wanawake maarufu namba 51 ni Pope Joan.

Hata katika karata za kale za Kirumi kuna karata zenye maandishi “La Papessa”—ikimaanisha “Papa Mwanamke”.

pope-joan-jpg.805196

Ukienda katika jiji la Siena sehemu inaitwa Duomo, kuna kanisa la kale la katoliki na ndani kuna sanamu za Mapapa 170. Mnamo karne ya 17 Kardinali Baronuis wa Vatican, ambaye alikuwa ni mtunza Library wa Vatican, aliwahi kuandika kuwa katika sanamu za Mapapa hao 170, mmoja wao ni Joan..Papa mwanamke. Baronuis akaendelea kuandika kuwa aliyekuwa Papa wa wakati huo alitoa amri kuwa sanamu hilo la Papa Joan liharibiwe, lakini hilo halikufanyika badala yake sanamu hilo likabadilishwa jina na juu yake likaandikwa Pope Zachary.

papacy-jpg.805197

Katika Basilica ya Mtakatifu Petro, ndani ya kanisa hili kuna michoro nane ya mwanamke inayomwonesha akiwa amevaa kofia na mavazi ya ki-Papa. Michoro hii maarufu ya zamani ilichorwa na Muitaliano Bernini.

Je Joan Anglicus alikuwa nani?

Joan Anglicus alizaliwa mwaka 814 huko Ujerumani katika kijiji kilichokuwa katika mji unaojulikana leo hii kama Mainz. Joan alikuwa ni binti mwenye kipaji na akili sana. Alizaliwa mtoto wa tatu na waliomtangulia walikuwa ni wavulana, mmoja alifariki akiwa na miaka 12, hivyo akabakia Joan na kaka yake aliyejulikana kama Johanes.

Miaka hiyo watoto wa kike walikuwa hawafundishwi kabisa kusoma, ni watoto wa kiume peke yao ndiyo walikuwa wanafundishwa kusoma na kuandika tena ni wale tu waliozaliwa katika familia za kifalme au wale waliozaliwa katika familia ambazo baba zao walikuwa kwenye mfumo wa kanisa la Rumi. Baba yake Joan alikuwa ni kasisi wa Kanisa Katoliki na kipindi hichi makasisi walikuwa wanaruhusiwa kuoa.

Joan alikuwa na akili sana na kipaji cha kutibu kwa kutumia miti shamba; ujuzi ambao alifundishwa na mama yake, lakini baba yake alikataa katu katu kumsomesha. Kaka yake alipopelekwa Ugiriki kujiunga na shule ya makasisi wa Kanisa katoliki, Joan akatoroka nyumbani na kumfuata kaka yake huko Ugiriki. Hapo shuleni makasisi wakataka kumkataa lakini akaonesha uwezo mkubwa sana wa kusoma na kuandika na kuielezea Biblia kiasi kwamba askari mkuu wa Ugiriki akavutiwa na kipaji chake na kusema kuwa atamtunza nyumbani kwake na kumsomesha hapo shuleni.

Baada ya Joan kumaliza shule, vita inatokea na kaka yake anauawa vitani. Baada ya vita kwisha Joan anaamua kujibadilisha jina na kujiita jina la kaka yake Johanes na kwenda kujiunga na chuo cha makasisi cha kanisa katoliki huko huko Ugiriki. Akiwa amejibadilisha jina na muonekano na kuonekana kama mwanaume, anajiunga na chuo hicho na kujifunza kila kitu mpaka anafuzu na kuwa kasisi kabisa.

Kutokana na kipaji chake cha kutibu magonjwa kwa kutumia mimea, Joan(Johanes) anapata umaarufu mkubwa sana kwani aliweza kuwatibu hata watu waliodhaniwa kuwa na ukoma. Inasemekana pia kuwa Joan alikuwa na nguvu za ajabu ndani yake.

Siku moja Joan akiwa kanisani hapo Ugiriki kama kasisi, aliugua na siri yake kidogo igundulike hivyo ikambidi atoroke na kuondoka. Akaondoka Ugiriki na kusafiri hadi Italia na kuingia Roma. Kiujanja ujanja akafanikiwa kuingia Vatican na kupokelewa kama Kasisi Johanes. Sifa zake za kuchapa kazi na kutibu wagonjwa zikaenea Vatican yote.

Siku moja aliyekuwa Papa wa wakati huo akaugua sana karibu ya kufa. Akaitwa Joan na kuja kumtibu na Papa akapona kabisa. Tokea wakati huo Papa akamchagua Joan kuwa msaidizi wake wa karibu na kumfanya kuwa Kardinali. Papa alipofariki Joan akachaguliwa kuwa Papa.

Joan alipochaguliwa kuwa Papa akaanza kubadilisha mwenendo wa kanisa kwa kuwasaidia sana maskini kwa kuwapa chakula maji na mahitaji yao muhimu. Kitu hichi kikamfanya Papa Joan kuwa maarufu sana kwa wakati huo hata akapewa jina na wenyeji wa Roma na kuitwa “Pope Populis”—yaani “Papa wa Watu”.

Stori ya Papa Joan ni ndefu sana lakini mwisho wa siku siri yake ilijulikana baada ya kupewa mimba na yule aliyekuwa mlezi wake ambaye alikuwa ni askari mkuu wa Ugiriki. Baada ya siri hii kujulikana Papa Joan alikufa wakati akijifungua mtoto wake tena alijifungulia njiani wakati akitembea kukagua jiji la Roma. Inasemekana alikufa wakati akijifungua na wengine wanasema aliuawawa kwa kupigwa mawe kwa kulitia aibu kanisa katoliki.

Mwaka 2009 watengenezaji wa filamu wa Ulaya, walitengeneza movie na kuiita “POPE JOAN”. Kwa wale wanaopenda wanaweza kuipata “movie” hii bure kabisa bila malipo kwenye mtandao huu hapa, https://solarmoviez.rukwenye search andika Pope Joan.

popejoan-jpg-b-jpg.805199Swali la kujiuliza hapa ni ikiwa Kanisa Katoliki linasema kuwa MUNGU ndiyo humchagua Papa, basi iweje Joan Anglicus aliweza kujipenyeza kiujanja na kuingia Vatican mpaka akachaguliwa kuwa Papa wakati yeye alikuwa ni mwanamke???

TOA MAONI YAKO IMETAYARISHWA NA WAHABARISHAJI MEDIA TEAM

Facebook Comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here