Mwanzoni kabisa, dunia ilikuwa ikitumia kalenda ya mtawala wa Kiroma aliyeitwa Julius Caesar. Kalenda hiyo ilianzishwa mwaka 46 Kabla ya Kristo. Kalenda hiyo ilikuwa na siku 465 na masaa 6.

Kalenda hiyo ilikuwa na makosa machache machache kwani hata sikukuu ya Pasaka ilikuwa mbele kabisa na si mwezi wa nne kama ilivyokuwa sasa hivi. Lengo kubwa la Papa Gregory XIII kuanzisha kalenda yake mwaka 1582 ambayo ndiyo inatumika mpaka sasa hivi ni kutatua matatizo madogomadogo yaliyokuwemo katika kalenda ya Caesar.

Baada ya Aloysus Lilius kutengeneza kalenda hii na kumpa Papa Gregory, haikuwa ikitumika kwanza, ilikuwa ikiwekwa vizuri na miaka mitano baadaye ndipo ilipoanza kutumika. Katika mwaka 1582, siku kumi ziliondolewa katika kalenda hiyo, yaani October 5 mpaka 14, kwa hiyo ikawa ikitoka October 4, kesho inakuwa October 15.

Baada ya kalenda ya Gregory kutolewa, hakukuwa na mataifa mengi yaliyoipenda, hivyo ilikuwa ikitumika katika nchi ya Italia, Spain na Ureno, sehemu nyingine bado walikuwa wakitumia ile ya Caesar ikiwemo Uingereza ila ilipofika mwaka 1752 ndipo Uingereza nayo ikaanza kutumia kalenda hiyo.

Tangu nchi ya Saudi Arabia ilipoanzishwa mwaka 1932 haitumii kalenda ya Gregory, Kalenda yao inaitwa Hijri (Kalenda ya Kiislamu) lakini kwenye kuwalipa wafanyakazi mbalimbali, hutumia kalenda hii ya Gregory.

Kalenda hiyo ya Kiislamu ina siku 354, pungufu ya siku 11 kutoka katika kalenda ya Gregory. 

WATU WALILALAMIKA SANA

Wakati Gregory anaanzisha kalenda yake, alizikata siku 11 kutoka katika kalenda ya Caesar. Jambo hilo lilileta malalamiko makubwa kwa watu waliokuwepo kipindi hicho kwamba je, wao watajua wamezaliwa siku gani na wakati kalenda haiwaonyeshi.

Hilo halikujibiwa, Vatican ikakaa kimya kwani walijua waliokuwa wakilalamika, kuna siku wangekufa na maisha kwenda sawa katika matumizi hayo ya kalenda hiyo. Ndivyo ilivyokuwa, kalenda haikubadilishwa, watu walipokufa, maisha yaliendelea kwa kutumia kalenda iliyokatwa siku mpaka leo hii.

KWA GREGORY, MWAKA MFUPI NA MREFU HUTOKEA SANA

Katika kalenda tunayoitumia leo hii, mara kwa mara mwaka 
unakuwa na siku 365 au 366 lakini katika kalenda ya Caesar, mwaka wenye siku 366 ulikuwa ukitokea kwa kila baada ya miaka minne.

Facebook Comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here