Lilith anayesemekana ni mke wa kwanza wa Adam… Hatajwi popote kwenye Biblia takatifu zaidi ya kwenye kitabu cha Isaya 34 : 14, na ambapo hata hivyo kutajwa kwake hakuna mahusiano kabisa na Adam

Kuna simulizi nyingi nje ya Biblia zinazokinzana na nyingine kushabihiana kumhusu mwanamama huyu Lakini zote zinakubaliana katika jambo moja kuwa Lilith alimwacha Adam kwakuwa hakutaka kuwa chini ya amri za mwanaume… Hakutaka kuongozwa wala kutawaliwa na mwanaume kwa utetezi kwamba, wote waliumbwa siku moja na kwa malighafi zinazofanana.. Hivyo hakuna mkubwa kuliko mwingine….

Sasa asili ya Lilith ni nini!? Ni wapi? 

Lilith anaonekana mara nyingi kwenye Biblia ya kiebrania na huko anajulikana kama malkia wa usiku, pepo katili la usiku lenye tamaa kubwa ya ngono… Huku kazi yake kubwa ikiwa ni kuiba watoto gizani usiku… Lilith sio jina jema popote zaidi ya kwenye imani za kipagani na kishetani.

Asili ya Lilith inatajwa sana kwenye simulizi za wayahudi (c 700-1000)… Hapa anatajwa kama mke wa kwanza wa Adam waliyeumbwa pamoja (mwanzo 1:27, kisha akafuatia mke wa pili wa Adam baada ya Lilith kuondoka (mwanzo 2:22)… Hapa inasemekana Lilith alimuacha Adam kwenye bustani ya Eden na hakutaka kurudi huko na kwenda kugawa kipochi manyoya kwa malaika muasi aliyeitwa samael…. Lakini pia simulizi nyingine zinasema aliondoka na kwenda kungonoka na shetani ili kuendeleza kizazi na uzao wa shetani…. 

Hii inaweza kuleta uhalisia kidogo kutokana na vile satanism wanavyomchukulia Lilith… Kumuamini na kumwabudu kama mungu mwanamke, mke wa baba yao shetani

Hizi zote ni simulizi nje ya Biblia takatifu lakini kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba kuna hicho kiumbe chenye jinsia ya kike kiitwacho Lilith ambacho hakuna popote kinatajwa kwa wema… Kuna mahali anaelezewa kama mchawi, pepo aliyengonoka na shetani kwa makusudi mazima ya kuendeleza kizazi chao kama tulivyoona hapo juu…. 

Facebook Comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here