Katika Karne ya 17, Kitabu cha Enoch kiligunduliwa katika Vitabu vitakatifu vya Madhehebu ya Ethiopian Orthodox na Coptic nchini Ethiopia na hadi kufikia Karne ya 19, kilikuwa kimeshatafsiriwa kwenye Kiingereza na kuushangaza ulimwengu wa Wakristo kwani kiliondolewa tangu zamani kwenye Nyaraka za kwenye Biblia.
Kuna mkanganyiko wa sababu zilizopelekea Kitabu cha Enoch kuondolewa kwenye Biblia, ikidaiwa siyo cha maandiko matakatifu. (?)
Kitabu cha Enoch, kimeeleza kuwa, chanzo cha kuanguka kwa Makaika/Sons of God/Watchers ni kitendo chao cha kuwatamani wanadamu na hivyo kupelekea Wana wa Mungu hao kuwafundisha Wanadamu elimuiliyokuwaimezuiliwakwa wanadamu:

 1. Kuwafundisha namna ya kutengeneza silaha – ilipelekea kutokea vita.
 2. Kuwafundisha wanawake urembo – ilipelekea tamaa za kimwili.
 3. Kuwafundisha elimu ya uaguzi (uganga).
 4. Kuwachukua wanawake na kuzaa nao – ilipelekea kuzaliwa majitu/giants waliotesa watu.

Baada ya Watoto wa Mungu kulala na wanadamu, watoto waliozaliwa walikuwa na maumbo makubwa sana. Walikuwa wanakula chakula kingi hadi Binadamu wakashindwa kuwatunza na hivyo giants hao wakawatenda vibaya wanadamu na kisha yakaanza kugeukia wanyama, ndege na samaki na baadaye yakageukana yenyewe kwa yenyewe hadi kuuana ili kunywa damu. Hapo ndipo Mungu akaamua kuleta gharika ili kuwafutilia mbali hao Giants baada ya kilio cha wanadamu kumfikia Mungu.

img_6607-jpg.844401

Biblia inaeleza kuwa Wana wa Mungu/Watchers waliona wanawakewazuri duniani na kulala nao. Lakini Kitabu cha Enoch kinaonyesha kuwa, hao Wana wa Mungu waliwafundisha wanawake namna ya kujiremba na baadaye ndipo waliwatamani. Je kipindi hicho cha Malaika kuwafundisha wanadamu walikuwa wanaishi wapi – duniani ama eneo fulani (mwezini/Mars)?

 • Kama Watchers hao waliwaona wanawake wakiwa duniani, je waliishi kwenye nyumba za kibinadamu ama chini ya Dunia (kwenye hollow earth)?
 • Kama Watchers waliwaona wanawake wakiwa nje ya Dunia, je walikuwa mwezini – “hollow moon” ama Sayari ya Mars (kituo cha mapumziko cha Anunnaki)?
 • Kama Malaika ndio waliowafundisha wanadamu urembo, je hiyo haimaanishi kuwa, walikuwepo kwa muda mrefu zaidi duniani kabla ya kuanza kufanya nao mapenzi na kuzaa giants/nephilim? (Fikiria kuwa, Anunnaki waliotoka Sayari ya Nibiru waliishi duniani – “Sumerian Civilization” bila kufa kwa karibia miaka 300,000 na waliondoka duniani kurudi Nibiru kuepa gharika, japokuwa wengine walibaki).
 • Mungu alimwadhibu Mwanadamu kwa kupunguza umri wake wa kuishi duniani hadi miaka 120 kutoka miaka hadi 900. Hata hivyo, kulingana na stories za watu waliowahi kuingia ndani ya Dunia (hollow), Binadamu wa kule ni giantsmore intelligent na wanaishi zaidi ya miaka 400. Je, hawa siyo waliosalimika gharika wakafanikiwa kukimbilia chini? Ama hao ndio Fallen Angels waliotupwa duniani baada ya kuasi huko duniani?
img_6471-jpg.845261

Kihistoria:
Mwanadamu ametumia miaka ipatayo 3,000,000 kutokea katika hatua ya Jamii za Nyani (Australopithecus) hadi kufikia kuwa Binadamu kamili (Homo Sapiens). Cha ajabu katika miaka yote hiyo 3,000,000 – 20,000 BC, Mwanadamu alifanikiwa kugundua yafuatayo pekee: zanazamawe(3,000,000), moto (250,000) na lugha (50,000). Hata hivyo, kati ya mwaka 15,000 – 10,000 pekee, Mwanadamu alipata maendeleo ya haraka haraka sana hasa kwenye kilimo, ufugaji na makazi (Neolithic Revolution). Kipindi hicho, Mwanadamu aligundua yafuatayo:

 • Upandaji wa mbegu kondeni.
 • Kumwagilia mashamba maji.
 • Ufugaji wanyama: mbwa, ng’ombe, mbuzi, kuku, bata, ngamia, punda etc.
 • Mgawanyo wa majukumu
 • Biashara.
 • Makazi ya kudumu (vijiji).

Haikupita muda, kufikia 3,500 BC, kukaibuka kwa Civilisation ya kwanza duniani – Sumerian Civilisation (chini ya Anunnakis), ikifuatana karibu karibu na Egyptian Civilisation (chini ya Sirians). Cha ajabu ni kuwa, Civilisations hizo na nyingine kubwa kubwa ikiwemo Mayan Civilisation, zina uhusiano wa moja kwa moja na hawa Aliens.
Najua watu wengi mnafahamu uvumbuzi ulioletwa na Civilizations hizo za kwanza lakini muhimu zaidi ni elimu ya kuandikakuhesabu na kalenda. Hata hivyo, Wataalamu wanakiri juu ya uwepo wa akili isiyo ya kawaida kukadiria kwa usahihi Kalenda ya miezi 12 ya siku 30/31 ama siku 365 za mwaka.
Tangu hapo, Dunia (Nje ya Afrika) haikuwahi kusinzia tena kwani Dola baada ya Dola ziliibuka (baada ya Civilisations za kwanza kupita) na kuendelea kwa kasi kubwa.
Tumeshaona Civilisations za Waarabu, za Wazungu, za Waamerika (Red Indians) na za Waasia. Katika Races zote duniani, tumebakia tu sisi Blacks (Negroids) ambao hatujawahi kuongoza mbio za ustaarabu duniani. Hata hivyo, tumeona Wahindi Weusi (Dravidians) nchini India wakiongoza mbio za maendeleo nchini India na wanaonekana wakiiongoza Dunia katika electronics na mathematics. 
When will we Negroids attain technological supremacy? Mhhh!! let’s wait and see or else we Negroids never benefited from Aliens’ DNAs.

img_6721-jpg.845260

Facebook Comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here