Wachawi mara nyingi hufanya kazi katika ulimwengu wa roho yaani ulimwengu ambao huwezi kuuona kwa macho ya kimwili.

Kwahiyo ili kuuona ni lazma uwe na macho ya kichawi au macho ya kiroho,Wachawi huanza kazi yao pindi inapofika saa 6 usiku ambapo hukutana katika vilinge(madhabahu) vyao ambapo kilinge hicho huwa ni mti mkubwa sana kwa ajili ya ibada kabla ya kwenda kuwanga. 

Kazi kubwa ya vilinge ni makutanio na katika kukutanika huko ndipo hupeana majukumu mbalimbali ya siku hiyo,inawezekana hata wew mtaani kwenu kipo kilinge lakini usikifahamu na sifa moja ya kilinge huwa ni jina lake kuwa maarufu na hubeba jina la sehemu husika mfano mwembe yanga,mwembetongwa,mbuyuni hiyo ni mifano michache tu ya vilinge kwa maana hubeba jina la sehem husika.

Pia wachawi huwa kuna siku ambayo hukutanika mara moja kwa mwezi kwa ajili ya kutatua shida zao mfano: kuongezewa nguvu na mkuu wa kilinge ambaye huwa ndio kiongozi wao ambaye huwapangia majukumu napia kushtakiana wao kwa wao maana pia hukopeshana misukule na nyama za watu.

Kwahyo wakishatokaga kwnye kilinge safari za kwenda kuwanga huanza ambapo hutumia usafiri mbalimbali kama ungo,fimbo,kijiko,fisi n.k katika kazi ambazo hufanya mara nyingi hupewa maagizo na viongozi wao ambao hao viongozi hupewa na mungu wa dunia hii ambae ni ibilisi moja kwa moja kutoka kuzimu na miongoni mwa hizo kazi ni kuhakikisha wanawasambaratisha wahubiri wa kikristo hasa wale wenye nguvu mfano kama marehem mzee kulola na pia kuhakikisha makanisa yote ya kiroho hayastawi maana vita kubwa ya shetani ni juu ya makanisa.

Kwa maana huamini kwmba kupitia watu wengi wanapookoka wao hujipunguzia wafuasi,kwahiyo hii ndio vita kubwa na majukumu makubwa sana ambayo ndio wamepewa wachawi na pia hii ndio vita ngumu sana kwao siku zote.

Pamoja na kazi zao zingine kama kuua,kufungia watu riziki zao na pia kuwatupia magonjwa lakini hiyo kazi ya kuua makanisa ndio kazi ngumu sana kwao.

Wachawi hutumia majini hasa jini anaeitwa khaurat kwa ajili ya usafiri ambapo kwa rank za usafiri mchawi anaetumia fimbo au bakora au kijiko huyo huwa ananguvu sana na huo ndio usafiri wa haraka kuliko usafiri wowote duniani,mchawi anaetumia ungo huyo ni mwanga au mchawi mdgo na hao ndio waliojaa uswahilini hao mara nyingi huwa na uwezo mdgo kinguvu.

Mchawi anapoanza safari ya kwenda kuloga ikiwa atapita juu ya nyumba yako wakati anaelekea kuloga na wakati wa kurudi itamlazimu apitie hapohapo kwako alipopita mwanzo maana huanza kuloga kuanzia saa 6 usiku ambapo ndio huanza shughuli zao na mwisho wa kuloga huwa ni saa 10 na nusu usiku ikizidi sana saa 11.

Wachawi wote duniani wameipitisha siku ya ijumaa kutokufanya safari yoyote ile ya kichawi au la ikitokea kwa dharula kwasababu siku ya ijumaa hupata vipingamizi sana vya safari zao kwa maana ijumaa mara nyingi walokole hufanya mikesha kwenye makanisa yao kwahiyo pindi wanapoomba na kusema kwao wachawi hupata shida sana na wakati mwngne hupata ajali au kupata ulemavu na hata kufa baada ya nguvu yake kuzidiwa na nguvu za Walokole wanapokuwa kwnye maombi yao na ndio maana unakuta mara nyingi wanaodondoka huwa ni wachawi wadogo wanaotumia ungo kwa maana wao nguvu zao huwa nindogo tofauti na wale wanaotumia fimbo au fagio ambao wenyew huweza kupata ulemavu.

Kwahiyo sasa ikiwa mchawi atapita kwao saa 7 ukiwa umelala na wakati anarudi saa 10 akute unaomba au mnafanya maombi basi tambua kwamba lazma atapata shida sana ndio maana walokole huwa wanaamka usiku wa manane kuomba maana husema vita vyao si vya damu na nyama(mwili) kama dini nyingne bali wao vita vyao nivyakiroho dhidi ya falme za wachawi,majeshi ya pepo wabaya na wakuu wa giza.

Ndio maana huomba sana kwa kukemea nguvu zote za giza,pia mchawi anapokutupia ugonjwa huwa ni sawa na ugonjwa halali kwa dalili na hata unapoenda hospital kupima hukuta ni ugonjwa huo ndio maana mtu anapoenda kanisani kuombewa na kuponywa mhubiri anaposema kwa jina la Yesu ugonjwa flani toka basi ugonjwa huo moja kwa moja hurudi kuzimu mahali ambapo hutengenezwa kwa maana magonjwa ya kichawi hutengenezwa kuzimu kwahyo yanaporudi huko huwa ni kama ni mzgo uliorudi kwa hasara.

Shetani yupo duniani kwa ajili ya kutesa watu ili kupitia mateso hayo watu wamfuate ndio unakuta mtu akishafungiwa riziki zake hujikuta anaenda kwa mganga kupata utajiri au kupata nyota na tayari anakuwa keshakuwa mfuasi na shetani anafahamu kabsa kwmba tayari keshahukumiwa ila sasa hataki kuangamizwa pekeyaana anatafuta wafuasi ili aangamizwe nao.

Facebook Comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here