News Bahrain, UAE zasaini makubaliano ya kuwekeana ubalozi na Israel

Bahrain, UAE zasaini makubaliano ya kuwekeana ubalozi na Israel

-

 

Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu na Israel zimesaini makubaliano ya kihistoria ya kuwa na uhusiano wa kibalozi, katika sherehe iliyosimamiwa na rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House mjini Washington. 

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema hatua hiyo inaweza kuwa mwanzo wa kumaliza kabisa uhasama kati ya nchi yake na mataifa ya kiarabu. 

Waziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu Abdullah bin Zayed Al-Nahyan amemsifu Netanyahu, akisema amechagua amani kwa kusitisha unyakuaji wa ardhi za Wapalestina. 

Wapalestina wameyapinga makubaliano hayo, wakiyaita usaliti uliofanywa na mataifa ndugu ya kiarabu. Hata kabla ya kusainiwa, makubaliano hayo yalipingwa pia na Iran pamoja na Uturuki. 

Hadi sasa, Misri na Jordan yalikuwa mataifa pekee ya kiarabu yenye uhusiano wa kibalozi na Israel.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

France MPs condemn UAE, Bahrain, Israel normalisation deals

A group of 61 French members of parliament said the ‘peace deals’ signed between Gulf states the UAE and...

2 Job Opportunities at Solidaridad, Senior Project Officers

 Solidaridad is a global civil society organization (CSO) that...

Zarif Pays Tribute to Fallen Heroes of Iran’s 8-Year Sacred Defense

- Society/Culture news - “We commemorate our fallen heroes—40 yrs after Saddam’s invasion & start of 8 yr...

Persepolis Loses to Al-Duhail in ACL 2020

- Sports news - Persepolis entered the Matchday Five fixture knowing a win would keep the team top...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you