Sport Michezo (Swahili) Manara amalizana na TFF, ni baada yeye Bumbuli na...

Manara amalizana na TFF, ni baada yeye Bumbuli na Hanspope kupigwa ‘rungu’

-

Mara baada ya Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwatoza faini ya shilingi milioni tano kila mmoja Msemaji wa Simba, Haji Manara na Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli na Mjumbe wa Kamati ya Sheria ya shirikisho hilo, Zakaria Hanspope.

Mchana wa leo, Haji Manara ameonekana katika ofisi za makao makuu ya TFF kulipa faini hiyo aliyopigwa na Kamati ya Maadili.

Klabu ya Simba imeposti kipande cha video ambacho kinamuonyesha, Manara akiwa amewasili katika ofisi za TFF na maburungutu ya fedha ili kulipa faini hiyo.

”Afisa Habari wa klabu, Haji Manara leo mchana amefika kwenye ofisi za Shirikisho la Soka nchini (TFF) kulipa faini ya milioni 5 ambayo alipigwa na Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo.”- Imeandika klabu ya Simba.

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliwatoza faini ya shilingi milioni tano kila mmoja Msemaji wa Simba, Haji Manara na Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli na Mjumbe wa Kamati ya Sheria ya shirikisho hilo, Zakaria Hanspope kutokana na makosa mbalimbali ya kimaadili huku wakitakiwa kutotenda kosa lolote la kimaadili ndani ya miaka miwili.

Mashauri yaliyokuwa yakiwakabili wadau hao wa soka ni kama ifuatavyo;

HAJI MANARA: Amekutwa na hatia kwa kuingilia majukumu ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji wakati wa kesi ya mchezaji Bernard Morrison kwa maneno aliyoyatoa kupitia Wasafi Media.

HASSAN BUMBULI: Amekutwa na hatia ya kusema uongo kwa Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji kwamba hawajapeleka nakala ya hukumu ya kamati wakati nakala ilifikishwa kwenye klabu yake siku moja kabla ya yeye kuongea na Wasafi Media.

ZAKARIA HANSPOPE: Amekutwa na hatia katika makosa mawili
(1) Kutoa taarifa ya muenendo wa shauri ambalo lilikuwa linajadiliwa huku yeye akiwa ni mjumbe wa kamati hiyo.

(2) Kuchochea umma kuhusu sakata la mchezaji Bernard Morrison.

Kamati hiyo imesema rufaa ziko wazi.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Why petroleum marketers will not join planned strike – IPMAN

The National Executive Council of the...

NCC boss, Danbatta, bags prestigious Zik Prize

Prof. Umar Danbatta, the Executive Vice...

‘I’m ready to honour police invitation’ – Gbagi reacts to four Delta hotel staff stripped naked

Former Minister of Education (State), Olorogun Kenneth Gbagi, on Saturday, reacted to the report that four staff of Signatious...

Job Vacancy KIGAMBONI at Kazini Kwetu Limited – Office Administrator

 Position: Office AdministratorLocation: Kigamboni, Tanzania, United Republic of OverviewOn behalf...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you