News Mgombea Ubunge wa ADC asema ataanza na walemavu

Mgombea Ubunge wa ADC asema ataanza na walemavu

-

- Advertisment -

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Wawi la kwa tiketi ya chama cha ADC Maryam Mohamed Muhene, amesema hamu yake kama akipewa ridhaa na wapiga wa Wawi, ni kuanza na kundi la watu wenye ulemavu, ili kuwaundia umoja wao na kuwapatia mitaji.

Alisema wapo viongozi kadhaa wa majimbo wameshapita ndani ya jimbo hilo lakini chakusikitisha ni kuona wanalisahau kundi la watu wenye ulemavu na kumaliza utumishi wao likiwa dhaifu.

Mgombea huyo wa ubunge ameeleza hayo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya sababu za kutaka apigiwe kura na kuwa mbunge wa jimbo la Wawi.

Alisema, kundi hilo la watu wenye ulemavu nalo ni sehemu ya jamii na linahitajia kufanya kazi kwa mujibu wa mazingira yao ili waondokane na utegemezi.

Alieleza kuwa, wakati umefika sasa kundi hilo kuliwezesha na kuibadilisha jamii mtazamo finyu kuwa watu hao wapo duniani kwa kuwa omba omba na wategeaji familia.

“Mimi kilichonisukuma hasa kuomba uongozi, kwanza ninauzoefu wa muda mrefu kuongoza, lakini kama wakinipa ridhaa wapigakura  wenzangu wa Wawi, basi kwanza kipaumbele ni kuanza na wenzetu wenye ulemavu,’’alifafanua.

Aidha alisema, katika kundi wapo wengine wenye ugonjwa wa akili, ambapo  hao kama akipata ridhaa atajenga nyumba maalum ya kuwahifadhi.

“Pamoja na kwamba wapo wagonjwa wa akili ambapo nilitarajia jamii iwasaidie, lakini ndio kwanza wanabakwa, sasa mimi nikirudi Jimboni nitawajengea nyumba na kuwahifadhi,’’alieleza.

Katika hatua nyingine mgombea huyo wa ubunge wa Jimbo la Wawi kwa tiketi ya ADC Maryam Mohamed Muhene, alisema kama wananchi wa Jimbo la Wawi watamuona anafaa na kumpa jimbo, anakusudia kuvifufua upya vikundi vya ushirika.

Alisema jengine ni kuona anatafuata mtaalamu na kuwapa wakulima mbali mbali namna bora ya kilimo na jinsi ya kuongeza mazao katika eneo dogo.

“Utaalamu wa kilimo bado mdogo sana, sasa kama nikiwa Mbunge nitatafuta mtaalamu ili wananchi wa Wawi walime padogo na kuvuna sana,’’aleleza.

Kuhusu uendeshaji wa kampeni, alisema hategemei sana ruzuku kutoka chamani kwake, bali amejipanga kuvitumia vyombo vya habaria na mtu mmoja mmoja kusambaza sera zake.

“Mimi nimeshajipanga kulitembea jimbo lote hata kwa mguu, maana inawezekana fedha za kufanyia kampeni zisiweko, lakini vijiji vyote vya Jimbo la Wawi nitavifikia na kuomba kura,’’alieleza.

Hivi karibuni mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ADC Hamad Rashid Mohamed, aliwaomba wapiga kwenye majimbo kadhaa walimosimamisha mgombea wa chama hicho, kuwapa kura ili kuimarisha maisha.

Alisema, ADC ikiingia madarakani vijana kadhaa watasahau kutafuta ajira serikali, na watajiegemeza kwenye kujiajiri iwe ni sekta ya uvuvi, kilimo au ufugaji.

“Hata wagombea wetu ubunge tumeshawaeleza kama wakipata riadhaa wahakikisha wanaimarisha maisha ya watu kwanza, iwe ni kilimo, ufugaji au biashara ndogo ndogo.

Omar Mjaka Kombo wa Wawi alisema chama chao ADC kimeamua kumsimamisha mwanamke kwa nafasi zote za ubunge na uwakilishi, wakiamini ni wachapa kazi.

“Wapiga kura wajitahidi kwa uchaguzi huu mkuu, kura zao wasijezipoteza kwa kuvipa vyama vyengine, bali wawatilie madiwani, mwakilishi, mbunge, rais wa Zanzibar na yule wa Jamhuri kupitia ADC,’’alieleza.

Hata hivyo Maua Makame Khamis ‘damaa’ na mwenzake Ashura Hija Maliki ambao hawataka vyama vyao vitajwe, walisema wameamua kwa hiari yao kuwaunga mkono wagombea wa ADC.

“Kwa vile hawa ni wanawake wenzetu na tunaamini wanazijua mno shida zetu, sasa kwa mwaka huu tutachana na vyama vyetu vya zamani na kuwapa kura mwakilishi na mbunge wa ADC,’’alifafanua.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania ‘NEC’ tayari imesharuhusu kwa wagombea ubunge na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanza kampeni zao.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

BREAKING: Lagos approves full reopening of churches, mosques

Lagos State Governor, Babajide Sanwo-Olu, has...

Girl Accidentally Exposes Nick Ruto’s Trip to Moi Hotel [PHOTO]

Details have emerged about Nick Ruto's trip to Lake Bogoria Spa Resort on September 5, 2020. In a photo that...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you