News Tanzia: Mwanasiasa mkongwe Salim Turky afariki dunia

Tanzia: Mwanasiasa mkongwe Salim Turky afariki dunia

-

 

Mwanasiasa mkongwe na Mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar, Salim Turky, amefariki usiku wa kuamkia Septemba 15 akiwa Hospitali ya Tasakhta Global Zanzibar baada ya kuugua ghafla

Turky alizaliwa Februari 11, 1963, alikuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae tangu 2010. Amefariki akiwa Mwenyekiti wa Kampuni za Turky zinazoendesha biashara zake Tanzania Bara, Zanzibar na Visiwa vya Comoro

Ikumbukwe kuwa mwaka 2017 Tundu Lissu aliposhambuliwa kwa risasi, Turky alitafuta ndege iliyompeleka Lissu Nairobi na kuwa Mdhamani wa Deni la kukodi ndege iliyokuwa inamilikiwa na FlyghtLink

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, Turky pia alijitokeza kutetea Ubunge katika Jimbo la Mpendae kwa tiketi ya CCM. Alifahamika zaidi kwa jina la ‘Mr White’

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

JCPOA Still Alive, US Must Know Era of Bullying Over, Iran’s FM Says

- Politics news - “Iran never hesitates to engage in negotiations, but will not renegotiate an issue that...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you