News Umoja wa Mataifa wasema ukosefu wa chakula umerudi tena...

Umoja wa Mataifa wasema ukosefu wa chakula umerudi tena Yemen

-

- Advertisment -

 

Mkuu wa misaada ya kiutu katika Umoja wa Mataifa ameonya kwamba uhaba wa chakula umerudi tena katika nchi iliyozongwa na machafuko ya Yemen. 

Mark Lowcock amezitaja Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu pamoja na Kuwait kama nchi ambazo hazijatoa msaada wowote katika kiasi cha dola bilioni 3.4 zinazohitajika mwaka huu. 

Lowcock amesema Umoja wa Mataifa ulilimaliza tatizo hilo nchini Yemen mwaka jana kwa kuwa wafadhili walitoa haraka michango iliyofikia asilimia 90 ya kiwango jumla kilichoombwa. 

Mkuu huyo amesema maisha ya mamilioni ya watu yaliokolewa kwasababu misaada iliongezwa. 

Ila kwa sasa anadai kwamba ni asilimia 30 tu ya kiasi cha pesa kilichoitishwa ambacho kimetolewa na kwamba Wayemen milioni tisa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa chakula, maji na matibabu.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

CEO Opens up on Struggles With Rent

The Covid-19 pandemic has left a number of individuals in the country in various sectors of the economy vulnerable, unable to...

Delta State govt gives updates on resumption of tertiary institutions

The Delta State Government says tertiary...

Iran, Turkey Discuss Ways to Boost Transportation Cooperation

- Economy news - In a post on his Twitter, Farazmand said, “(In a meeting with) Turkey’s Transport...

VIDEO: Mgombea Ubunge ajitoa kwenye kinyang’anyilo cha Uchaguzi, mwenyekiti wake ajiuzulu

Mgombea wa Ubunge Jimbo la Madaba mkoani Ruvuma kupitia Chama cha NCCR-MAGEUZI bwana Mkinga Ugin Gidion,amejitoa kwenye nafasi ya...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you