News Wabunge wa Uingereza waunga mkono muswada wenye utata

Wabunge wa Uingereza waunga mkono muswada wenye utata

-

 

Wabunge wa Uingereza wameunga mkono muswada wa sheria ambao utakiuka baadhi ya vipengele vya makubaliano yaliyoafikiwa baina ya nchi hiyo na Umoja wa Ulaya, kuhusu mchakato wa Uingereza kuondoka katika umoja huo marufu kama Brexit. 

Hatua hiyo imefikiwa licha ya malalamiko makali kutoka kwa maafisa wa Umoja wa Ulaya, na upinzani kutoka kwa mawaziri wakuu wa zamani wa Uingereza na pia baadhi ya wanachama maarufu wa chama tawala cha Conservative. 

Muswada huo unaohusu sera ya soko la ndani la Uingereza ulipata kura 340 za kuunga mkono, dhidi ya 263 zilizoupinga, na kwa ushindi huo umepata ridhaa ya kujadiliwa kwa undani mnamo wiki hii na inayofuata. 

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema muswada huo ni muhimu kuhakikisha usalama dhidi ya alichokiita vitisho vya Umoja wa Ulaya kuliwekea vikwazo vya kiushuru soko la ndani la Uingereza.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Murder of Plateau monarch: Lalong, Gyang direct hunt for killers

Governor Simon Lalong of Plateau State has assured that the killers of a traditional ruler, Da Bulus Chuwang Janka,...

Navy flags off Exercise AKERE in Bayelsa

The Central Naval Command, on Wednesday,...

Mkongo wa Taifa wa mawasiliano waunganisha visiwa vya Pemba na Unguja

 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeweka saini ya mkataba wa makubaliano...

Wananchi mkoani mtwara kupata maji safi na salama

 Na Faruku Ngonyani, Mtwara.Mkurugenzi wa Ubora wa Maji kutoka Wizara ya Maji Mhandisi Philipo Chandy amesema kuwa wananchi Mkoani...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you