Health TATIZO LA HERNIA. - Doctor JOH

TATIZO LA HERNIA. – Doctor JOH

-

Hernia ni uvimbe (eneo lililotuna) kutokana na viungo vya ndani ya
mwili kusukuma kuta za misuli inayozunguka au kushikilia viungo hivyo.
Hernia hutokea wakati kuna udhaifu au kuna tundu kwenye kuta za misuli
inayoshikilia na kuviweka viungo vya tumbo kwenye sehemu yake
(peritoneum). Udhaifu huo unaweza kuviruhusu viungo vya ndani kusukuma
na kupenyeza, na kujenga eneo lililotuna. Unaweza kuwa na hernia ikiwa
unaweza kuhisi namna ya eneo laini lililotuna kwenye maeneo ya tumbo au
kinena au kwenye kovu ambalo lilitokana na upasuaji. Eneo hili
lililotuna linaweza likapotea ukiminya sehemu hiyo au ukijilaza. Unaweza
kupata maumivu kwenye eneo hilo hasa ukikohoa, ukiinama au ikinyanyua
kitu kizito.

Hernia ni tatizo linalowasumbua watu wengi katika nchi nyingi
duniani. Hernia mara nyingi hutokea kwenye maeneo ya tumbo, lakini
huweza pia kutokea kwenye sehemu ya juu ya mapaja, kwenye kitovu, na
kwenye maeneo ya kinena. Hernia haihatarishi maisha mara moja, lakini
haiwezi kuondoka yenyewe na inaweza kuhitaji kufanyika kwa upasuaji.
Hernia mara nyingi hupewa majina kutokana na sehemu ya mwili
inapojitokeza, ingawa mara nyingine majina huweza kutolewa kutokana na
sababu nyingine za kuitambulisha. Kila hernia hutibiwa tofauti na
nyingine kutokana na sehemu iliyopo na sababu nyingine za kitaalamu.
Kuwa na elimu ya kutosha ya kila aina ya hernia itakusaidia kujua namna
ya kutoa maamuzi sahihi ya tiba yake.

Aina Za Hernia

1. Inguinal (groin hernia)

Inguinal hernias au groin hernias hutokea pale utumbo au mafuta
yanaposukuma na kupenya kwenye misuli ya eneo la kinena. Hii ndiyo aina
ya hernia inayowasumbua watu wengi zaidi. Inguinal hernia inaweza
kuonekana kwa wanaume na wanawake lakini huwapata zaidi wanaume kwa
sababu tayari wana kijitundu kidogo kwenye misuli ya kinena kwa ajili ya
kupitisha arteri, veni na mrija wa mbegu vinavyoelekea kwenye korodani.
Asilimia 97 ya aina hii ya hernia huonekana kwa wanaume.

Inguinal-Hernia-Bulges

Hernia inaweza kuwa juu ya misuli ya tumbo (direct inguinal hernia)
au inaweza ikafuata njia ya mrija wa shahawa pale unapoacha eneo la
tumbo na kuelekea kwenye korodani (indirect inguinal hernia). Inguianal
hernia huanza kama uvimbe mdogo ambao huongezeka na muda. Uvimbe
unaoonekana ni utumbo au mafuta yanayosukuma misuli.

uvimbe wa inguinal hernia

Uvimbe huweza kupotea kwa kulala na kurudi mwili ukianza shughuli.
Uvimbe huu ukiwa mkubwa sana, huenea kutoka kwenye kinena hadi kwenye
korodani zenyewe. Hernia ikiwa kubwa sana huleta matatizo kuiondoa.
2. Umbilical (belly button hernia)
Belly button hernia au umbilical hernia kama inavyoitwa mara
nyingine, ni pale utumbo au mafuta yanapopenya kupitia sehemu dhaifu ya
misuli iliyopo katikati ya tumbo chini ya kitovu. Sehemu hii ndiyo
inayopata udhaifu mara nyingi kwa sababu ndiyo sehemu inayopata
minyumbuko zaidi wakati tukifanya shughuli yo yote ya mwili.
Umbilical hernia inaweza kuwa moja kwa moja chini ya kitovu, lakini
wakati mwingine inaweza kuwa juu kidogo au chini kidogo ya kitovu.
Inaweza kuonekana kama kijikokoto kidogo chini ya ngozi, au ikikua
inaweza kuonekana kama kijimpira cha gofu au hata kufikia kimpira cha
tenisi kama kikiachwa bila tiba.

umbilical hernia - henia ya kitovu
Kwa watoto wa kufikia hadi miaka 5, hernia hii kwa kawaida huondoka
yenyewe. lakini kwa watu wazima hernia hii haipungui na huwa inazidi
kuwa kubwa kila wakati. Wanawake kwa kawaida hupata umbilical hernia
wakati wa ujauzito, na hupotea yenyewe baada ya kujifungua. Kwa baadhi
ya wanawake, kijishimo hiki katika musuli hubakia baada ya kujifungua.
Inashauriwa kuwa wanawake wasubiri kwa miezi 3-6 kuona kama hernia hii
itafunga yenyewe.
Kama ilivyo kwa hernia nyingine, dalili za kawaida ni maumivu kwenye
kitovu. Kutokana na mafuta au misuli kupita kwenye hernia hii, uvimbe
utaonekana chini ya ngozi kwenye eneo hilo. Baada ya muda, kama hernia
itakuwa kubwa sana, utumbo unaweza kunaswa kwenye hernia hiyo na kuleta
madhara kwenye utumbo, vikiambatana na kichefuchefu, kutapika, na
kufunga choo.
Kwa sababu hakuna hernia inayopona yenyewe, upasuaji unahitajika.
Njia inayopendekezwa hapa ni open surgery kwa sababu tundu ni dogo.
3. Femoral (below the groin)
4. Epigastric (just below the breast bone)
5. Ventral (above the umbilicus)
6. Incisional (through a prior surgery site)
7. Sports
 
Namna nyingine za kuelezea Hernia:
1. Recurrent (after a prior hernia repair)
2. Unilateral (one side of the body)
3. Bilateral (both sides of the body)

Sababu Za Hernia

Ukiondoa hernia inayotokana na upasuaji wa awali, mara nyingi hakuna
sababu inayoeleweka ya kusababisha hernia. Watu walio kwenye hatari
zaidi ya kupata hernia ni wenye umri mkubwa, na wanaume wapo kwenye
hatari zaidi kuliko wanawake.

Hernia inaweza kujitokeza mtoto anapozaliwa au kwa watoto waliozaliwa na dosari kwenye kuta za matumbo yao.

Shughuli au madawa yanayosababisha mgandamizo kwenye kuta za tumbo vinaweza kusababisha hernia. Vitu hivi ni pamoja na:

. Kujikamau kwa nguvu wakati wa haja kubwa kutokana na choo kuwa kigumu
. Kikozi cha mara kwa mara
. Kuwa na tatizo la cystic fibrosis
. Kuvimba kwa tezi dume
. Unene wa kupindukia
. Kukojoa kwa shida
. Kunyanyua vitu vizito
. Maji tumboni
. Lishe duni
. uvutaji wa tumbaku
. Korodani zisizoshuka
. Uchovu wa mwili

Dalili Za Hernia

Mara nyingi, hernia ni uvimbe unaoonekana usio na mauvimu na
usiohitaji tiba ya haraka. Lakini wakati mwingine, inaweza kukukosesha
raha na kuwa na maumivu, dalili zikiongezeka wakati umesimama au wakati
unanyanyua vitu vizito. Watu wengi huona uvimbe ukizidi na hatimaye
humwona daktari.

Kuna wakati ambapo hernia inahitaji huduma ya haraka ya upasuaji, kwa
mfano, pale sehemu ya utumbo inapokuwa imezibwa na hernia ya tumbo
(inguinal hernia).

Hatua za haraka za uchunguzi zinatakiwa zichukuliwe wakati inguinal hernia inapoanza kuonyeza dalili kali za:

. Maumivu
. Kusikia kichefuchefu
. Kutapika

Uvimbe wa hernia yenye dalili hizi mara nyingi ni mgumu na huleta maumivu na hauwezi kusukumwa urudi ndai ya tumbo.

Hiatal hernia inaweza kuleta dalili za acid refluc kama kiungulia, kinachotokana na tindikali za tumboni kupanda kwenye koromeo.

Tiba Ya Hernia

Hernia isipokuwa na dalili mbaya, njia bora ni kuiacha na kusubiri,
ingawa hii inaweza kuwa njia sahihi kwa hernia za ina fulani, kama
femoral hernia.

Madaktari bado hawajafikia kukubaliana wote kuhusu faida za kufanya
upasuaji kwa inguinal hernia ambayo haijaanza kuleta usumbufu ambayo
inaweza kusukumwa ndani ya tumbo. Madaktari wengi wa nchi ya Marekani
wanashauri kusubiri badala ya kufanya upasuaji. Wengine wanashauri
kufanya upasuaji ili kuiwahi kabla haijaweza kuziba sehemu za utumbo.

Uamuzi wa kufanya upasuaji unategemea hali iliyopo, pamoja na sehemu
hernia ilipo, ambapo kuna upasuaji wa aina mbili unaoweza kufanyika:

. Open surgery
. Laparoscopic operation (keyhole operation).

Open surgery huziba hernia kwa kutumia nyuzi (sutures), mesh au vyote
na kidonda juu ya ngozi kuzibwa kwa nyuzi, staples au surgical glue.

upasuaji wa hernia wa laparoscopic

Laparoscopic repair hutumika kwa upasuaji wa kujirudia ili kukwepa
makovu, igawa ni ghali zaidi, inapunguza uwezekano wa kuleta madhara
hasa ya maambukizi ya vijidudu.
Kwa kulinganisha upasuaji huu wa aina hizi mbili, asilimia za
uwezekano wa hernia kujirudia zinalingana, ingawa open surgery inaweza
kusababisha madhara zaidi, kama maambukizi ya vijidudu.

Tunaomba maoni yako kuhusu mada yetu ya leo na usisite kuuliza swali
lo lote ulilo nalo kuhusiana na mada hii. Tunaahidi kukuijibu kwa wakati
mzuri,

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

October School Reopening: Parents Anxious of Increased Charges

Parents across the country have grown anxious fearing increased charges after Covid-19 Education Response Committee settled on Monday, October 19 as...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you