Health MAUMIVU YA TUMBO KATIKATI YA MZUNGUKO WA HEDHI

MAUMIVU YA TUMBO KATIKATI YA MZUNGUKO WA HEDHI

-

Je unapata maumivu ya tumbo chini ya kitovu
au kwenye kinena siku za katikati ya mzunguko?.kama unapata hali hii unapata
hali kitaalam inaitwa MITTELSCHMERZ.

MITTELSCHMERZ ni maumivu yanayotokea
kwenye   tumbo sehemu ya chini ya
kitovu,kwenye kinena au kwenye nyonga kipindi unapokuwa siku za katikati ya
mzunguko.yaani siku ambazo yai linakaribia kuachiliwa au linapoachiliwa kutoka
kwenye vifuko vya mayai (ovari)

Kwa lugha nyingine tunaweza kusema ni maumivu
ya tumbo na nyonga wakati wa siku za hatari.

Asilimia 20% ya wanawake wanapatwa na hali
hii.

Nini kinasababisha hali hii.

Kikawaida kwa mwanamke yai huachiliwa wiki
2 tokea kuanza kwa hedhi.mabadiliko ya hormone yanayotokea kipindi hiki
huchochea mifuko ya mayai (ovari) na kupelekea kufanya yai lililokomaa kupasua
utando unaolizunguka ili liachiliwe kutoka kwenye mfuko wa yai (ovari). Yai
hili linatoka na majimaji yaliyokuwa yanalizunguka na pia damu.

Kitendo cha yai kupasua utando ili litoke
hupelekea maumivu kidogo ya tumbo (mittelschmerz)

Pia maji maji yanayotoka pamoja na yai
kutoka kwenye ovari yanaweza kusababisha kuta za mirija ya uzazi (fallopian
tubes) kupata michomo (inflammations) na kupelekea kupata maumivu haya.

DALILI

Mamivu mithili ya kichomi au tumbo kukaza
sehemu ya chini ya kitovu. halii pia inaweza kuambatana na kuona damu kidogo
ukeni (spotting)

Hali hii uisha ndani ya masaa 24 hadi 48.

MATIBABU

Hali hii sio tatizo la kiafya, ni hali
inayotokana utendaji kazi wa mfumo wa uzazi.

Unaweza kutumiw njia zifatazo kupunguza
hali hii inapokupata

1.kujikanda tumbo sehemu ya chini ya kitovu
na maji ya moto inasaidia kuondoa/kupunguza hali hii

2.kutumia dawa za kutuliza maumivu

3.massage ya tumbo

Muda gani umwone daktari

1.endapo maumivu ni makali sana

2.imeambatana na homa

3.hali hii ikitokea kwa muda unaozidi siku
3

4.ikiambatana na kutoka uchafu ukeni wenye
harufu

Karibu ujifunze zaidi mambo mbali mbali
yanahusu hedhi katika seminar yetu kwa njia ya mtandao.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Govt to Offer 1Million Unemployed Youth Jobs

The government is working to solve the high unemployment rate in the country by offering jobs to one million...

October School Reopening: Parents Anxious of Increased Charges

Parents across the country have grown anxious fearing increased charges after Covid-19 Education Response Committee settled on Monday, October 19 as...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you