BASATA yawapongeza Diamond, Rayvanny na Nandy kushinda Tuzo Marekani

0
26

Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), limetoa pongezi za dhati kwa Wasanii Nandy, Rayvanny pamoja na Diamond Platnumz kwa ushindi wa Tuzo ya African Entertainment Awards USA 2019(AEAUSA)na kuliletea Taifa heshima.

Taarifa iliyotolewa na Basata imeeleza kuwa hii  ishara kwamba wasanii hao wanakubalika ndani na nje ya Tanzania, hivyo basi Ushindi huu uwe ni fursa ya kupanua wigo wa kazi zao kuingia katika soko la kimataifa Zaidi.

Diamond Platnumz ameshinda tuzo ya African Entertainment Awards USA (AEAUSA) kwenye kipengele cha ‘Best Collaboration Award’ kupitia wimbo wake wa Baila.

Advertisements

Huku Rayvanny na Nandy kwenye vipengele vya Best Male/Female in East, South and North Africa.

Pia Mtangazaji wa kituo cha Times FM, Lil Ommy naye ameshinda tuzo ya ‘Best Host’, Huku Babu Tale akichukua tuzo ya Meneja bora wa wasanii barani Afrika.Facebook Comments