Health IMANI POTOFU KUHUSU VVU/UKIMWI - Doctor JOH

IMANI POTOFU KUHUSU VVU/UKIMWI – Doctor JOH

-


Ukimwi ni ugonjwa unaosababishwa na ukosefu wa Kinga mwilini, ugonjwa
huu husababishwa na virusi vya ukimwi(VVU).  
Hadi sasa, bado hakuna tiba ya ugonjwa wa Ukimwi, lakini kuna dawa
zinazotumika kupunguza makali ya ugonjwa huu (ARV), hivyo matumizi ya
mapema ya ARV yatakuwezesha kuishi ukiwa na afya njema, na ndiyo sababu
tunahimizwa sana kupima afya zetu ili kujitambua na kuchukua hatua
mapema.

Ingawa maarifa ya ugonjwa huu ni mengi, ila bado kumeendelea kuwa ni
changamoto kubwa katika jamii yetu na nchi nyingine zinazoendelea. MOja
ya changamoto hizi ni imani potofu iliyojengeka katika jamii
inayopelekea watu ama kuwanyanyapaa wagonjwa wa Ukimwi au kuogopa kupima
kwakuwa wakishajulikana watanyanyapaiwa. Hii, hurudisha nyuma harakati
za mapambano ya ugonjwa huu.

Leo hii tuangalie imani potofu juu ya ugonjwa wa ukimwi.

Hauwezi kuambukizwa au kumuambukiza mtu virusi vya ukimwi kwa njia zifuatazo

  • Kuumwa na mbu
  • Kwa jasho
  • Kuchangia vyoo, sauna, vifaa vya gym, bwawa la kuogelea
  • Kuchangia taulo
  • Kwenda shule pamoja au kuwa na rafiki mwenye virusi vya ukimwi
  • Kupiga chafya au kukohoa
  • Kushikana mikono, kukumbatia au kupigana busu kavu na mtu mwenye virusi vya ukimwi
  • Kuvuta hewa moja na mtu mwenye virusi vya ukimwi

Imani nyingine potofukatika jamii ni kama

Kupata maambukizi ya ukimwi ndiyo mwisho wa maisha, hii si kweli, kwa kupima na kujitambua mapema na kuanza ARV mapema, kutakupelekea kuishi maisha marefu yenye afya njema.

Unaweza kumtambua muathirika kwa kumuangalia afya yake au muonekano wake kwa macho.
Hauwezi kumtambua muathirika kwa kuangalia kwa macho, watu wengi hawana
dalili yoyote ya maambukizi ya ukimwi kwa miaka ya awali. Hivyo, njia
pekee na ya uhakika kujua kama mwenza wako ana maambukizi au la ni
kupima. Na, sasa hivi upimaji wa HIV umerahisishwa zaidi na unatolewa
bila gharama yoyote.

Tohara kwa wanaume inazuia kabisa maambukizi ya ukimwi: Ukweli ni kuwa, tohara inapunguza hatari ya maambukizi ya virusi ya ukimwi kwa kiasi kikubwa kama, lakini si kweli kwa inazuia maambukizi.

Ukimwi unatibika: Hadi sasa bado hakuna tiba ya
ugonjwa wa Ukimwi.  ARV husaidia kupunguza makali ya virusi vya ukimwi.
Hivyo , matumizi bora ya ARV hupelekea virusi kufubaa na kushindwa
kuzaliana hivyo kumuwezesha mtu anayeishi na virusi vya ukimwi kuisha
maisha marefu na yenye afya lakini si kweli kwamba zinatibu ugonjwa wa
Ukimwi.

Nikiwa nina VVU/Ukimwi sitakiwi kubeba ujauzito: Unao uwezo wa kupata mtoto ili mradi viwango vya virusi (Viral load)
ipo chini na imechungwa vyema ndani ya miezi sita. Wenza ambao mmoja
wao ana maambukizi na mwingine hana, wanao uwezo wa kutumia njia ya
tendo kwa ajili ya kupata ujauzito lakini wanatakiwa kuzingatia viwango
vya virusi (viral load). Hivyo, unashauriwa kupima na kuongeza
na washauri nasaa (Daktari) watakaofuatilia uwingi wa virudi na
kukushauri muda muafaka wa kushika ujauzito.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

TANESCO yaboresha hali ya umeme Uru Kilimanjaro

 Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea na uboreshaji hali ya upatikanaji wa umeme (voltage improvement) maeneo mbalimbali nchini ikiwemo...

Qatar yapinga madai ya kuiunga mkono Israel

Katika mfumo wa maazimio ya kimataifa, Qatar imethibitisha msimamo wake thabiti wa kukomesha uvamizi wa Israeli kwa ardhi ya...

NTV Visits Viral Kids Impersonating Their Anchors [VIDEO]

They say that all it takes to stand out is unique content and as it looks, H-Town Kids, popular...

Govt to Offer 1Million Unemployed Youth Jobs

The government is working to solve the high unemployment rate in the country by offering jobs to one million...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you