Afisa Elimu awalaumu wazazi kuwaficha wanaosababisha mimba

0
10

Na Adelina Kapaya, Katavi.

 Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi Enelia John awalaumu wazazi kutotoa ushirikiano pale mwanafunzi anapobainika kuwa na ujauzito.

Ameyasema hayo wakati kamati ya Kudhibiti ukimwi manispaa ya Mpanda ilipotoa takwimu ya wanafunzi waliopata ujauzito Octoba 2019 na wanafunzi 18 walibainika kuwa na ujauzito kutoa shule ya kashauriri na kasimba.

Enelia amesema wazazi hawatoi ishirikiano pindi serikali inapotaka kuwabaini  watu wanaosababisha mimba na kuwaaminisha watoto kutosema mtu aliempa ujauzito wengi wao  wakidai kuwa hawawafahamu.

Hata hivyo wamekua wakijitaidi kufuatilia kesi hizo  kwa wazazi ambao wanatoa ushirikiano kuhakikisha waharifu wanabainika na sheria kufuata mkondo wake

Mwenyekiti wa Halmashauri ya manispaa ya mpanda Deodatus Kangu ameshangazwa na takwimu hizo na amewataka madiwani kushirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha watu hao wanapatikana.

“Nilitendo ambacho sijapendezwa Nacho kwa idadi ya wanafunzi waliopata mimba ndani ya mwezi mmoja halafu waliosababisha  hawapo ni kitendo cha aibu sana”

Miongoni mwa  wanafunzi waliopata ujauzito wanne ni wakidato cha nne ambao wangetakiwa kuhitimu mwaka huu.