ATHARI ZA MWANGA WA BLUE KIAFYA.

0
31

Naposema mwanga wa blue wengi watafikiria
ule mwanga unaotoka kwenye taa za blue,Ila sio huo naouzungumzia hapa.

Mwanga
tunaoona kutokea kwenye jua,taa,simu
nk inakuwa ni muunganiko wa mawimbi ya umeme-sumaku (electro magnetic
waves).
Mawimbi haya yanaposafiri huzalisha nguvu. Mawimbi yakiwa mafupi ndo
huzalisha
nguvu nyingi zaidi na mwanga wenye mawimbi marefu unakuwa na nguvu
kidogo. Kila urefu wa mawimbi unawakilishwa na rangi na hapo ndipo
tunapata makundi mbali mbali mfano X ray,gamma rays, ultra violet rays.

Katika aina za mawimbi hayo ya mwanga macho
yanaweza kuona baadhi (visible light).

Mwanga wa blue (blue light) mawimbi yake ni
mafupi (short wave length) kwa hiyo unazalisha nguvu kubwa. Kuwa katika mwanga
wa blue kwa muda mrefu ina madhara kiafya hasa kwenye macho na mfumo wa
usingizi (circadian rythm)

VYANZO VYA MWANGA WA BLUE.

mwanga wa blue upo kila sehemu. Mwanga wa
jua unakuwa pia na mwanga wa blue ndani yake. Vyanzo vingine ni TV,simu, taa za
ndani mfano tube lights nk.

Kwenye mwanga wa jua unakua na mawimbi
marefu hivyo kusababisha madhara ni kidogo sana. Kwenye vifaa kama TV na
Simu,Computer na Tablets mwanga huu unakuwa na mawimbi mafupi hivyo ni rahisi
sana kusababisha madhara.

Katika lens ya macho kunakuwa na seli za
kukinga mwanga huu usiharibu macho japo kinga hii haiwezi kustahimili kiwango
kikubwa cha mwanga huu.

MWANGA WA BLUE UNAATHIRI VIPI AFYA.

mwanga huu unapokuwa kwa kiwango kikubwa na
kwa muda mrefu husababisha uharibifu kwenye lens ya jicho na kupelekea matatizo
ya macho.

Katika mwili kuna kichocheo kinachoitwa
melatonin hii ni hormone inayosaidia kuweka utaratibu wa kusinzia  na kuamka (circadian rythm). Hormone hii ndio
inatuwezesha kutambua usiku ni muda wa kulal na mchana muda wa kuwa macho.
Mwanga wa blue husababisha ubongo kupunguza uzalishaji wa hormone hii hali
inayopelekea mtu kupata shida kwenye swala la kusinzia. Kwa ufupi inapelekea
tatizo la kutopata usingizi endapo unakua na tabia ya kutumia vitu vyenye
mwanga wa blue muda mfupi kabla ya kulala.

Tafiti zinaonesha kuvurugika kwa mpangilio
wa kusinzia na kuamka (circadian rythm) inapelekea mwili kuzalisha hormone ya
stress (cortisol ) kwa wingi hali ambayo inapelekea kuvurugika kwa hormone
nyingine za mwili mfano hormone za uzazi.

NINI CHA KUFANYA.

Ni
vyema kupunguza exposure ya mwanga huu
wa blue hasa muda wa lisaa kabla ya kulala.epuka kuangalia simu au TV
ndani ya nusu saa kabla ya kulala ili kuepuka kuharibu mpangilio wa
uzalishwaji wa hormone ya melatonin inayosaidia tupate usingizi. Kwa
sasa hivi TV za kisasa na
baadhi ya simu zinakuwa na jinsi ya kuzuia mwanga huu (blue light
filter). Kama
simu yako ina blue light filter basi vyema usiku uweke katika mode hiyo
ili
kuepuka madhara ya mwanga huu.