Benzema aipandisha kileleni Real Madrid

0
4

Karim Benzema akipongezwa na wenzake baada ya kufunga mabao mawili dakika za 17 na 29 kwa penalti katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Eibar kwenye mchezo wa La Liga leo Uwanja wa Manispaa ya Ipurua.

Mabao mengine ya Real Madrid yamefungwa na Sergio Ramos dakika ya 20 kwa penalti na Federico Valverde dakika ya 61 na kwa ushindi huo kikosi cha kocha Zinadine Zidane kinapanda kileleni katika La Liga, kikifikisha pointi 25, tatu zaidi ya mabingwa watetezi, Barcelona.