Chama cha NCCR-Mageuzi chatangaza kujitoa kwenye Uchaguzi

0
15

Chama cha NCCR-Mageuzi kimetangaza kujitoa kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.

Msimamo huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia jijini Dodoma akiongea na Wanahabari.

Ikumbukwe tayari CHADEMA, ACT Wazalendo na CHAUMA wameshatangaza kujitoa kwenye uchaguzi huo.

Hata hivyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amesema Mamlaka ya Uchaguzi inawatambua wagombea wa vyama vya upinzani vilivyotangaza kujitoa kwenye Uchaguzi huo.