DC Matinga awataka Halmashauri kupambana na uharibifu wa mazingira

0
17

Na Adelina Kapaya, Katavi.

Advertisement

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Lilian Matinga  amewataka halmashauri ya wilaya ya Mpanda kutoa maeneo maalum kwa ajili ya shughuli ya kufyatua matofali ili kupunguza uharibifu wa mazingira na kutohatarisha maisha ya watoto.

Akiwa katika kikao cha balaza la madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ametoa agizo kwa Halmashauri kuhakikisha wanawadhibiti wanafyatua matofali karibu na makazi ya watu kwani kwa  msimu wa masika maji hutuama katika shimo wanalochimba Kwa ajili ya kutafuta udongo na kuhatarisha maisha ya watoto na kuwasababishia mauti.

Matinga amesema kuwa ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anamlinda mtoto hivyo kama manispaa wahakikishe shughuri za kufyatua tofari zinasitishwa ili kuwasaidia watoto

Aidha Matinga amewataka kuhakikisha wanaweka bikoni katika mipaka ya maeneo ya taasisi ili kupunguza migogoro baina ya halmashauri na wananchi wanaoishi   karibu na taasisi hizo

Mwenyekiti wa halmashauri hio William Mbogo ameongezea kwa kuwataka madiwani na watendaji kuhakikisha wanapunguza mimba za utotoni  kwa kuwashughurikia wanaosababisha mimba hizo

Halmashauri ya manispaa ya mpanda inajumla ya kata 15 na miongoni mwa kata ya kakese imekua na tatizo la mimba za utotoni takribani watoto 65 walipata mimba na mmoja akiwa ni Mwanafunzi na mtuhumiwa ameshahukumiwa miaka 30 kutumika kifungo

Na madiwani  wamebainisha changatanoo mbalimbali wengi wao ikiwa ni kukosa ofisi ya kata na kata 7 ndio zenye ofisi kati ya kata kumi na tano(15)Facebook Comments