Diamond atoa somo kwa Wanafunzi

0
5

Kuelekea tamasha la Wasafi (Wasafi festival), msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametembelea Shule ya Msingi Mwongozo kwaajili ya kutoa msaada na elimu ya virusi vya ukimwi.

Tukio hilo limetokea Alhamisi hii, ambapo baadhi ya shule za sekondari za jirani zimehudhuria ambazo Shule ya Sekondari ya Kambangwa Shule ya Sekondar Hananasifu, Shule ya Sekondari Turiani, Shule ya Sekondari Mzimuni na Shule ya Sekondari Makumbusho.

Akizungumza na wanafunzi hao Diamond amewataka kuongeza juhudi katika masomo yao na kujiepusha na mambo mabaya ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya ili waweze kutimiza ndoto zao.

“Wasanii wengi wanatokea katika Wilaya ya Kinondoni hivyo jitahidini muyashikilie mazuri kuliko mabaya, mkitaka kufanikiwa zingatia kile unachokifanya, hapa kuna historia ya mambo ya mihadarati nisingependa kuwaona na nyie mkiingia huko,” amesema Diamond.

Kwa upande wake Mratibu wa Shughuli za kudhibiti ukimwi Halmashauri ya Kinondoni, Roby Gweso amewataka wanafunzi kuachana na tabia ya kutumia madawa ya kulevya na kuepuka vishawishi ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.