Hivi ndivyo Vyama 11 vya upinzani visivyosusa uchaguzi wa Serikali za mitaa

0
10

Vyama 11 vya upinzani visivyo na uwakilishi katika Bunge la Tanzania vimetangaza kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.

Vimetangaza uamuzi huo leo jijini Dar es Salaam siku moja baada ya Chadema kujitoa kushiriki uchaguzi huo.

Vyama hivyo ni DP, NRA, AFP, Demokrasia Makini, UDP, ADC, Ada- Tadea, Sauti ya Umma (Sau), TLP, CCK na UMB

Vimesema vitashiriki vikiamini Wizara ya Tamisemi inayosimamia uchaguzi huo itatenda haki kwa kuwarejesha wagombea wake walioenguliwa kushiriki uchaguzi huo.

“Tunaamini watarudishwa kwasababu wamekidhi matakwa. Tunataka tushindane kwa hoja na sera kwenye mikutano ya hadhara,” amesema katibu mkuu wa DP, Abdul Mluya kwa niaba ya viongozi wa vyama hivyo.