Madaktari zaidi ya 200 wafukuzwa kazi Zimbabwe

0
14

Serikali ya Zimbabwe imewafukuza kazi madaktari 200 kwa kosa la kufanya mgomo.

Chombo kinachoshughulikia huduma za afya nchini Zimbabwe kimesema madaktari 211 wamefukuzwa kazi juma hil kwa sababu ya mgomo unaoendela kudai malipo mazuri ya mishahara.

Madaktari walikutwa na hatia ya kutokuwepo kazini bila likizo wala sababu muhimu” kwa siku tano zaidi kw mujibu wa taarifa ya Bodi ya huduma za afya (HSB)

Mgomo ulianza mwezi Septemba.

Bodi hiyo imesema karibu theluthi tatu ya madaktari wote yaani madaktari 516 kati ya 1,601 walioajiriwa kwenye hospitali za serikali wamechukuliwa au watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Chama cha madaktari wa hospitali nchini Zimbabwe hakijasema chochote kuhusu taarifa hizi mpya, lakini awali walilalamikia vitendo vya vitisho, shirika la habari Reuters limeripoti.

Mgomo huo umesababisha kuzorota kwa huduma katika hospitali kubwa, ni huduma za dharura pekee ndizo zinazotolewa.

Serikali imesema haiwezi kugharamia ongezeko la mishahara wakati ambao raia wa Zimbabwe wanahitaji suluhu ya haraka ya kuondokana na kile wanachokiita mauaji ya taratibu ya kimbari, ameeleza mwandishi wa BBC mjini Harare, Shingai Nyoka.

Zimbabwe iko kwenye hali mbaya kiuchumi na gharama za maisha ziko juu kiasi cha kuathiri vipato vya watu.

Mshahara wa daktari unakadiriwa kuwa kiasi cha pauni 80 kwa mwezi.

”Kwa saa tunacholipwa hakitoshelezi kwa chakula wala kodi ya nyumba,” alisema daktari Lindsey Robertson akikiambia kipindi cha Newsday cha BBC mwanzoni mwa wiki hii.