Manula afunguka baada ya kuachwa Taifa Stars

0
7

Imeelezwa kuwa kipa wa klabu ya Simba, Aishi Manula amesema anaheshimu maamuzi ya kocha Mrundi, Ettiene Ndayiragije kutomuita katika kikosi cha Taifa Stars.

Siku kadhaa zilizopita Ndayiragije alitangaza kikosi cha Stars ambacho kitacheza mechi za kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Libya na Equatorial Guinea.

Manula ameeleza kuwa kutoitwa kwake wala haiwezi kumkatisha tamaa kwani ni maamuzi ya kocha na anachukulia jambo la kawaida.

Kipa huyo ameongeza kuwa kwa sasa yupo fiti asilimia 100 na anawatakia kila la kheri wachezaji wenzake ambao wameitwa kwa ajili ya mechi hizo mbili.

Manula amekuwa hana bahati ya kuwa sehemu ya kikosi hicho tangu aitwe mara moja wakati Stars ikiwa na kibarua cha kufuzu CHAN dhidi ya Kenya.