Mbunge ataka kipaumbele sekta ya kilimo

0
9

Mbunge wa Nanyamba (CCM), Abdalah Chikota imeomba Serikali kuweka kipaumbele katika sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na kuzitengea fedha Halmashauri kwa ajili ya kujenga maghala, jambo ambalo litasaidia kuokoa zaidi ya Sh. bilioni moja kwa mwaka.

Akichangia mjadala huo Chikota, amesema kuwa kwa sasa uhifadhi wa mazao umekuwa ukifanyika kwenye maghala ya watu binafsi na kuwa kama halmashauri zitawezeshwa kujenga maghala kutaokoa fedha nyingi.

Amesema kwa sasa kilo moja ya mazao imekuwa ikihifadhiwa kwa gharama ya Sh.38 hivyo kwa tani 30,000 zinagharimu Sh. bilioni moja kila mwaka.

Alisema ili kuokoa fedha hizo ni lazima serikali itenge fedha kwa ajili ya kujenga maghala hayo hususani ya mazao ya pamba na korosho ili kuepukana na matumizi ya fedha hizo.

“Tutenge fedha kwa na kuzipatia mamlaka za Serikali za mitaa ili kujenga maghala hayo, hii itasaidia kuachana na gharama tunayoitumia kuhifadhi mazao katika maghala ya watu binafsi, badala yake tutaongeza mapato ya Seikali,” amesema Chikota.