Mbunge wa CCM aliesema wahudumu wa ATCL hawana mvuto ajibiwa ‘hatuajiri kuonyesha sura’

0
13

Baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Husna Mwilima kusema wahudumu wa ndege za ATCL hawana mvuto kwa wateja, shirika hilo limesema haliwachagui kwa ajili ya kuonyesha sura.

“Hatuchagui wanawake kwa ajili ya kuwapeleka kuonyesha uzuri kuna vigezo lazima tuwapime uelewa. Lazima kujua wana uwezo upi wa kufuatilia mafunzo watakayopewa ili watoe huduma inayotakiwa kwa wateja wetu na si sura,” alisema Ladislaus Matindi, mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Jana bungeni mjini Dodoma wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo mwaka 2020/2021, Mwilima aliwaponda wahudumu wa ATCL kuwa hawana mvuto.