Meya Ilala apokea AC mbili kutoka kwa Azim Dewji kwaajili ya kituo cha Afya Buguruni Mnyamani

0
9

Msitahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto amewataka wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono katika jitihada za kuwaletea wananchi maendeleo.

Kumbilamoto ametoa rai hiyo mara baada kupokea Ac mbili kutoka kwa Azim Dewji zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi (10) ambazo zimefungwa katika kituo Cha afya Buguruni kwa Mnyamani.

“Kipekee Sana nichukue fursa hii kumshukuru bwana Azim Dewji kwa moyo wa dhati ambapo huduma za upasuaji zilishindwa kuanza kwa kuwa chumba hakikuwa na AC lakini kwa Sasa huduma zitaanza muda wowote kuanzia week ijayo” alisema Msitahiki Meya.

Aidha kwa upande mwingine mstahaiki amewataka wananchi kutumia fursa hiyo kwa huduma za upasuaji kituoni hapo zitatolewa bure mara baada ya Rais John Magufuli kutoa vifaa vya upasuaji katika kituo hicho.