Mtu mmoja akamatwa na gramu 270 za Heroini Mashariki mwa Uturuki

0
6

Mtu mmoja akamatwa  na gramu 270 za madawa ya kulevya katika operesheni ilioendeshwa Mashariki mwa Uturuki.

Mtu  mmoja aripotiwa kukamatwa na jeshi la Polisi  la kupambana na madawa ya kulevya  katika operesheni ilioendeshwa Mashariki mwa Uturuki.

Mtu huyo amekamatwa akiwa na gramu 270 za heroini.

 Kulingana na taarifa zilizotolewa na jeshi la Polisi mkoani Van,  operesheni kali dhidi ya  walanguzi wa madawa ya kulevya  inaendeshwa katika pembe nne za mkoa huo.

Msako mkali umeendeshwa katika kitongoji cha  Hafiziye Ipekyolu baada ya kuripotiwa gari ambalo lilizua mashaka.