Polisi Tarime waua majambazi watatu

0
22

Na Timothy Itembe Mara.

Askari wa Jeshi la polisi Tarime/Rorya wamefanikiwa kuua majambazi watatu kati ya watano waliokuwa wakivamia Nyumbani kwa mzee Daudi Ogutu Novemba 07,2019.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake kamanda mkoa wa kipolisi Tarime,Henry Mwaibambe alisemakuwa tukio hilolilitokea majira ya saa4 usiku Novemba 2019 katikakijiji cha Obwere Shierati wilayani Rorya.

“Askari polisi juzi wamefanikiwa kuua jambazi moja huku wakijeruhi wengine wawili kati ya watano waliokuwa wamevamia nyumbani kwa mzee Daudi Ogutu kwa lengo la kuiba na kupora mali ambapo kati ya majeruhi wawili Kesanta Chacha 19 mkazi wa Mjini Tarime alipatikana na kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo na kufanikiwa kumpata majeruhi mwingine  John Marwa Kitare ambapo walifariki dunia wote wakiwa njiani wakipelekwa  hospitalini ili kupatiwa huduma ya matibabu”alisema Mwaibambe.

Mwaibambe aliongeza kuwa katika eneo la tukio polisi walifanikiwa kuokota maganda matano ya risasi na  mengi ya kiwa ya Silaha aina ya CGM pamoja na Shooti Gani.

Polisi wetu baada ya kufanikiwa kumkamata majeruhi Kisanta Chacha alitoa ushirikiano wa kuwapeleka Askari wetu kwenye  eneo la tukio ambapo majambazi hao walikuwa wamemficha jambazi mwenzio  moja ambaye jina lake halijafahamika ambapo Askari walikuta mwili wa jambazi huyo akiwa amekufa tayari,tunatoa wito kwa ndugu jamaa waliopotelewa na Mtu wao kwenda Hospitali ya Shirati kuona mwili wa Marehemu ili kuutambua na kuuchukua kwa ajili ya mazishi aliongeza kusema Mwaibambe.

Katika tukio hilo Asjkari Polisi wakifanikia kuwanyang’anya silaha aina ya bunduki mbili zenye magazine moja na risasi saba pamoja na kufanikiwa kuokota maganda ya risasi matano aliongeza kusema Mwaibambe.

 Mwaibambe alimaliza kwa kusem kuwa Polisi hao wamefanikiwa kupata Bundiki Mbili moja iliyotengenezwa kienyeji yenye mitutu miwili kwa pamoja na AK-47 na Magazine moja na risasi saba ikiwemo maganda matano ya risasi na ganda moja la bunduki aina ya Shoot Gani.

Mwaibambe ametumia nafasi hiyo kuwataka  wananchi wa Tarime/Rorya kuendelea kutoa taarifa pindi watakapo waona majambazi wawili waliokimbia wakiwa na Bunduki aina ya Shooti Gani ili kukamatwa na kupelekwa kwenye sheria.