Rwanda yatafuta soko la kimataifa la maua

0
10

Kampuni za maua nchini Rwanda zinalenga kupanua soko lao la kimataifa kwa kushiriki katika Maonyesho makubwa ya Kimataifa ya Maua (IFTF).

Maonyesho hayo ambayo yameingia mwaka wa 10 sasa tangu kuanzishwa yalifunguliwa jana nchini Uholanzi, huku Rwanda ikishirikia kwa mara ya tatu sasa.

Uholanzi ndio soko kuu la maua duniani na kwa kiasi kikubwa mchangiaji mkuu wa mauzo ya nje ya maua ya Rwanda kwa asilimia 98.

Maonyesho hayo ya siku tatu yanaileta pamoja sekta ya maua duniani, huku yakilenga kuongeza uzalishaji na matumizi.

Mwaka huu Rwanda inashiriki ikiwa na malengo ya kukuza sekta ya maua ya nchi hiyo, matokeo yaliyokusudiwa ni athari chanya kwa mauzo na mahitaji ya maua ya Rwanda kupitia soko la mnada wa maua la Uholanzi.