Vibanda vyateketea kwa moto soko kubwa Mpanda

0
9

Na Adelina kapaya, Katavi.

Baadhi ya vibanda vya wafanyabiashara soko  kubwa Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi vimeteketea kwa moto huku chanzo kikiwa bado hakijajulikana.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa mnamo saa 6 usiku wa kuamkia tarehe10  waliona moto ukiwaka na walijitaidi kuokoa baadhi ya bidhaa zilizokuwemo kwa kushirikiana na jeshi la zimamoto na kuokoa vitu vichache na vingine kuteketea kwa moto.

Kaimu msimamizi wa jeshi la zimamoto Israel Mtika  amesema bado upelelezi unaendelea ili kujua chanzo cha moto na bado hawajatathimini vitu vilivyo teketea kwa moto.