VIDEO: Vyama vilivyojitoa kwenye uchaguzi vyaonywa, waliohusika na vurugu wadakwa

0
17

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Robert Boaz amesema kuwa, hali ya uhalifu nchini hasa makosa makubwa ya jinai imepungua kwa kiasi kikubwa kwa asilimia 24.7 ukilinganisha na kipindi cha miaka ya nyuma, ambapo kushuka kwa takwimu za uhalifu kumechangiwa kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi, wadau wa amani na vyombo vya ulinzi na usalama.

DCI Boaz amesema kuwa, katika kipindi hiki ambacho tunaelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo katika mchakato huu kumeanza kujitokeza matukio mbalimbali ya uvunjifu wa amani ambayo kama yasipodhibitiwa sawa sawa yanaweza kuvuruga mchakato huo huku baadhi ya watu ambao wametajwa kutokuridhika wameharibu na kujeruhi watu wengine ambapo Jeshi la Polisi kamwe alitofumbia macho vitendo hivyo na tayari hadi kufikia sasa watu kadhaa wamekwisha kamatwa.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI…..USISAHAU KUSUBSCRIBE