Wananchi wamsimulia RC Mnyeti wanavyokula Kichapo kutoka kwa wafugaji

0
7

Na John Walter-Manyara

Wananchi wa Kijiji Cha Manyara  kata ya Magara Halmashauri ya Babati wamemlilia mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti kuwanusuru na wafugaji wa kabila la kimang’ati ambao wanawapa kichapo na kuchungia mifugo kwenye mashamba yao ya mazao.

Kilio hicho walikitoa kwa Mnyeti  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji Cha Magara.

Mkazi wa Kijiji Cha Manyara Athuman Bakari alisema wafugaji hao wamekuwa tishio kwa wakulima maana wanachungia mifugo yao kwenye mashamba yao na wakulima wakihoji wanachalazwa kakola na wengine kuchomwa mishale na mikuki.

Thadeo Lazaro alimwambia Mnyeti kuwa wafugaji hao wanawatuma watoto wakachungie kwenye mashamba alafu wao wanajificha vichakani wakiwahoji watoto kwanini wanachungia wazazi wanaibuka na kutoa kichapo kwao.

Lazaro alisema licha ya kuwa yupo katika nchi yake lakini hana amani muda wote anatembea na silaha akihofia wamang’ati hao kumuua huku wakiwaambia kuwa hayo mashamba hawatakaa wayalime kwa amani.

Akijibu malalamiko ya wananchi hao Mnyeti aliliagiza jeshi la polisi kufika Kijiji Cha Manyara na kuwasaka wafugaji hao huku aliwataka wananchi kushirikiana na polisi.

“Hawa mang’ati wana vichwa vigumu kuelewa, polisi tumia nguvu kidogo kuwaondoa na wengine unakuta wanaletwa na wanasiasa hivyo ondoeni hao haiwezekani wachungie mazao ya watu,”Alisema Mnyeti

Katika kukomesha uhalibifu unaofanywa na wafugaji hao wa kimang’ati Mnyeti alimtaka afisa mtendaji wa Kijiji hicho kuuza ng’ombe wao wale wafugaji wanaokaidi kuchangia michango ya maendeleo na kusumbua kijijini hapo.