Bunge la Marekani laendelea na hatua ya kumshitaki Rais Trump

0
10

Bunge la Marekani linaingia katika wiki muhimu ya kumshitaki rais bungeni, ambapo Wademocrat ambao walikuwa na matumaini ya kuwavutia Warepublican, sasa wanakabiliwa na uwezekano wa kutokea mgawanyiko mkubwa zaidi kwa misingi ya chama kuhusiana na suala la kumuondoa rais Donald Trump madarakani.

Wabunge walipitia kwa mara ya kwanza ripoti ya kumshitaki rais ya kamati ya bunge la ujasusi jana usiku kwa faragha, na mwenyekiti Adam Schiff amesema kuwa ripoti hiyo itatolewa rasmi leo.

Maelezo katika ripoti hiyo yanatarajiwa kujenga kesi ya chama cha Democratic dhidi ya Trump kuwa alihusika katika kile Schiff anachokiita makosa na utendaji mbovu unaoweza kusababisha rais ashitakiwe, kwa kuishinikiza Ukraine kuwachunguza Wademocrats na Joe Biden wakati akizuwia msaada wa kijeshi kwa nchi hiyo mshirika.