CHADEMA washangazwa na Sumaye – MUUNGWANA BLOG

0
10

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kimeshtushwa kuona mwanachama wake ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye akitumia nembo ya taifa katika barua yake ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema kuwa chama hicho hakina taarifa za mkutano huo na kwamba wameona barua hiyo mitandaoni kama ilivyokuwa kwa wananchi wengine.

“Tunaona barua hiyo katika mitandao kama wengine, tumeshtushwa kuona barua yenye nembo ya Taifa inatumika kuitisha mkutano wa kiongozi wetu,” amesema

Ikumbukwe leo katika Mkutana wa Sumaye na Wanahabari alitangaza kuondoka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kusema kwa sasa atakaa bila chama.