Changamoto ya vifungashio RUNALI yaanza kutatuliwa

0
8

Na Ahmad Mmow, Nachingwea.

Changamoto ya uhaba wa vifungashio vya korosho katika chama kikuu cha ushirika cha RUNALI, mkoani Lindi imeanza kutatuliwa.

Hayo yameelezwa leo na meneja mkuu wa RUNALI, Jahida Hassan alipozungumza na Muungwana Blog mjini Nachingwea.

Jahida alisema changamoto hiyo ambayo imesababisha korosho nyingi kushindwa kufikishwa  maghala makuu kutoka maghala ya vyama vya msingi (AMCOS) imeanza kutatuliwa baada ya chama hicho kupokea gunia 90,000.

Alisema gunia hizo zimeanza kusambazwa leo kupelekwa kwenye AMCOS zinazounda chama hicho. Ambazo zipo katika wilaya za Nachingwea, Liwale na Ruangwa.

Meneja huyo alisema licha ya gunia hizo. Lakini pia wanatarajia kupokea gunia nyingine 220,000 ndani ya wiki hii.

Kufuatia kupelekwa gunia hizo, meneja huyo ametoa wito kwa watendaji wa AMCOS waharakishe kuandaa taarifa na wapeleke kabla ya Jumapili ya wiki ijayo ili korosho zitakazofungwa kwenye gunia hizo ziwahi kuuzwa katika mnada wa sita utakaofanyika Jumapili ijayejpo.

Alisema gunia hizo zinauwezo wa kujazwa tani 7,200. Kwahiyo kunamatumaini makubwa katika mnada ujao korosho nyingi zitauzwa kuliko mnada wa tano ambao korosho zilizouzwa zilikuwa tani 2,111 wakati mahitaji ya wanunuzi yalikuwa takribani tani 11,000.