China yatangaza kuweka vikwazo dhidi ya kitendo hiki cha Marekani

0
4

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema, China itaweka vikwazo dhidi ya kitendo cha Marekani cha kusaini mswada wa haki ya binadamu na demokrasia ya Hong Kong na kuuidhinisha kuwa sheria.

Bibi Hua amesema, vikwazo hivyo ni pamoja na kusimamisha kuidhinisha ombi la Marekani katika kupumzisha manowari na ndege zake mkoani Hong Kong, na kuweka vikwazo dhidi ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya Marekani yanayochochea vurugu mkoani Hong Kong.

Ameihimiza Marekani kuacha kitendo chochote cha kuingilia kati mambo ya mkoa wa Hong Kong na mambo ya ndani ya China, kwani China itachukua hatua za lazima kulingana na hali halisi, ili kulinda kithabiti utulivu na ustawi wa mkoa wa Hong Kong, na kulinda kithabiti mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya China.