Faida zitokanazo na Mapera – MUUNGWANA BLOG

0
10

Mapera ni miongoni mwa matunda ya msimu lakini yenye ladha nzuri na yanapotumiwa vizuri huweza kuwa na manufaa kadhaa ndani ya miili yetu.

Leo naomba kukueleza hizi faida nyingine kadhaa kuhusu mapera.

1. Husaiida kuimarisha kinga za miili yetu kutokana na kuwa na vitamin C ya kutosha ndani yake.

2. Pia matumizi ya tunda hili humuweka mhusika kwenye uwezekano mdogo wa kukumbwa na matatizo ya saratani za aina mbalimbali.

3. Tunda hili pia ni tunda rafiki kwa wale wenye shida ya kisukari.

4. Husaidia kulinada afya ya moyo pia.

5. Aidha, tunda hili nalo ni rafiki kwa wenye shida ya kukosa choo.

6. Husiadia kuimarisha afya ya macho kutokana na kuwa na vitamin A ya kutosha ambayo huboresha uoni wa mhusika.