Frederick Sumaye ‘amtaja Mbowe’ kama sababu ya kuondoka CHADEMA

0
13

Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania, Frederick Sumaye ameeleza moja ya sababu ya kuondoka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ni kutotendewa haki pale alipotaka kugombea nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho.

Ameeleza hayo leo mbele ya Wanahabari ambapo amedai kuwa nafasi ya Uenyekiti ndani ya CHADEMA ni sawa na kuonja sumu.

“Nilipochukua fomu ya kugombea Uenyekiti CHADEMA Taifa tu nongwa zikaanza, mimi nilichukua fomu ili kuonesha kuwa Demokrasia ipo CHADEMA tofauti na maneno yanayosemwa mitaani kuwa ukigusa Kiti kile tu ni shida”.

“Nafasi ya Mwenyekiti Mbowe haiguswi mimi nilitaka kuonesha kuwa hilo sio kweli lakini nilikuwa najidanganya nimefanyiwa figisu kwenye uchaguzi wa kanda kisa niligusa kiti cha Uenyekiti Taifa,” alisema.

Aliendelea kwa kusema, “Mbowe aliwahi kutupa nasaha kuwa tusiionje sumu kwa kuilamba, na mimi siwezi kuigusa sumu kwa kuilamba leo natangaza rasmi kuwa sitoendelea kugombea kwenye nafasi ya Uenyekiti Taifa CHADEMA”.