Fredreck Sumaye aondoka na Kigogo CHADEMA

0
10

Mratibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pwani, Casmir Mabina amewasilisha barua makao makuu ya chama hicho ya kujiuzulu nafasi hiyo.

Ameeleza sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na yaliyotokea kwenye uchaguzi wa kanda hiyo ambayo yamemfanya aliyekuwa mgombea uenyekiti, Fredreck Sumaye atangaze kukihama chama hicho.

Leo kwenye mkutano na wanahabari, naye Sumaye ametangaza kuondoka ndani ya Chama hicho na kusema kwa sasa atakaa bila chama, huku akidai kujiunga upinzani si jambo rahisi, kwamba alikuwa akiandamwa na Dola pamoja na familia yake.

“Mimi siyo mwanachama wa Chadema kuanzia sasa na sijiungi na chama kingine cha Siasa kuanzia leo na niko tayari kutumika katika chama chochote hata Chadema katika kushauri” alisema Frederick Sumaye.