Hizi ndizo sababu za kuku kutotaga mayai

0
6

 Mara nyingi wafugaji wengi wamekuwa wakilalamika ya kwamba kuku wao wamekuwa hawatagi, na wengi wao wamekuwa hawajui sababu ni hizi ndizo sababu.

Kuku hupunguza utagaji na hata kuacha kutaga kabisa iwapo:-
Hawakupewa chakula bora au cha kutosha.
Hawapewi maji safi ya kutosha.
Wamebanana, yaani hawakai kwa raha.
Vyombo vya maji  au chakula havitoshi.
Mwanga hautoshi.
Majogoo yamezidi katika chumba(weka jogoo 1 kwa mitetea 10)
Kuku wanaumwa.
Wana vidusa vya nje na ndani (external and internal parasite).
Wamezeeka (umri zaidi ya miaka miwili na nusu).
Maumbile ya kuku mwenyewe.