Jinsi ya kumjua msichana ambaye hakupendi

0
20

Je, unataka kujua msichana havutiwi nawe? Kuna dalili
unahitaji kujua ili kuepuka uchungu wa kukataliwa baadaye 1. Anakataa kukupa
namba mara ya kwanza?

Ikiwa msichana hataki kukupa namba yake ya simu
unapomuomba mara ya kwanza, jua ya kwamba hakutaki. Ikiwa atakupa, itachukua
muda kufanya hivyo, jua kuwa hataki mambo yako, hivyo ni bora kukoma mapema kwa
sababu mtasumbuana bure tu. 

2. Amekupa namba isiyo yake? 

Msichana akifanya hivi huhitaji
kungoja sana kujua kuwa hapendezwi nawe. Kushinda ukimfuata itakuumiza bure tu
kwani simu zako zitakuwa zikichuliwa na mtu mwingine. Huenda akalaumu mfumo
mbaya ya mawasiliano. 

3.Hachukui simu unapompigia? 

Unangoja nini kujua hakutaki? Ikiwa msichana atachukua simu
mara moja unapopiga, jua ya kuwa anakupenda na ni ishara kuwa mtakuwa marafiki.
Lakini akichukua muda kujibu, kimbia

4. Hakutembelei?

Ikiwa hatembei kwako, basi ni ishara kwamba hataki kukuona.
Hakuna haja ya kumfuatafuata.

5. Ukisikia marafiki wake wakicheka unapompigia simu

Ikiwa atafanya hivyo, hiyo ni tahadhari, huenda anakudharau.
Utangoja mpaka akuvunje moyo? Endelea na maisha yake, utapata mwingine
anayekupenda.

6. Anapotumia pesa zako ovyo ovyo Baadhi ya wanawake sio
wema. 

Licha ya kuamua kutokuwa na uhusiano wowote nao, wanapenda
tu kutumia wanaume vibaya kwa kuwasaidia kuharibu pesa zao walizofanyia kazi
kwa bidii. Ikiwa hakupendi, ataandamana na marafiki wake wote unapomualika na
kukufanya kutumia pesa zaidi ya ulivyokuwa umepanga.