Katika wilaya hii migogoro haiishagi, jitahidini muimalize wenyewe – Rais Magufuli

0
28

Rais John Magufuli amewataka wananchi wa Misungwi na viongozi wake kuacha kuendekeza migogoro iliyokuwa imekithiri wilayani humo na badala yake wajikite kwenye kujiletea maendeleo.

Advertisement

Ameyasema hayo leo wakati wa uwekaji jiwe la msingi Ujenzi wa Daraja la Kigongo – Busisi lenye urefu wa 3.2 kilometa katika Ziwa Vitoria  litakalounganisha Mkoa wa Mwanza na Geita.

“Niwaombe mdumishe umoja maana katika wilaya hii migogoro haiishagi na haiwezi ikasuluhishwa na Rais hivyo jitahidini muimalize ninyi wenyewe, mna viongozi wa kila aina kaeni muimalize na kuangalia maendeleo ya mbele kwa eneo lenu kwasababu makundi hayatawasaidia kitu,” amesema Rais Magufuli.

Aidha kuhusu miradi iliyokwama na ambayo imeshindwa kutekelezwa kwa madai ya kupotea shilingi bilioni moja, Rais Magufuli amemuagiza waziri wa Ujenzi kufuatilia zilipo fedha hizo huku mawaziri wengine wakitakiwa kushughulikia matatizo yaliyotajwa.Facebook Comments