Kenya: Mvuvi aokolewa na Helikopta katika mafuriko

0
4

Mvuvi mmoja, Vincent Musila amenusuriwa kifo baada ya kukama kwenye kisiwa tangu siku ya Ijumaa kutokana na mafuriko makali.

Musila alikuwa amekwenda kuvua samaki kama kawaida katika mto mmoja mjini Thika katikati mwa Kenya wakati mto huo ulivyovunja kingo zake.

Watu wengi walitazama bila usaidizi wowote walipokuwa wakisubiri usaidizi wa dharura ili kumuokoa.

Zaidi ya watu 250 wamefaki na wengine milioni kuathiriwa na mafuriko na maporomoko katika eneo lote la Afrika mashariki. Takriban nusu ya vifo 120 vimetokea nchini Kenya huku zaidi ya watu 160,000 wakiathiriwa.