Klabu ya Zamalek ya Misri yamvuta kazi kocha wake

0
5

Klabu ya Zamalek ya Misri imeamua kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake mkuu Mserbia Milutin Micho baada ya kutopendezwa na matokeo mabovu ya timu yao.

Micho amefutwa kazi siku mbili baada ya kufungwa 3-0 na TP Mazembe mjini Lubumbashi Congo DR katika mchezo wa kwanza wa hatua ya Makundi ya michuano ya CAF Champions League.

Ikiwa ni kipigo cha pili mfululizo baada ya kufungwa tena 2-1 katika Ligi Kuu ya nchini Misri dhidi ya Enppi, Micho anafutwa kazi ikiwa ni miezi minne imepita toka asaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuinoa klabu hiyo Agosti 18.