Mkurugenzi na Wakala watema nyongo Ronaldo kukosa Ballon d’Or 2019

0
6

Huku Asilimia kubwa ya Wanafamilia wa soka wakiwa jijini Paris kushuhudia Lionel Messi, Megan Rapinoe, Alisson Becker na Matthijs de Ligt wakinyakua tuzo nne za Ballon D’or 2019, Cristiano Ronaldo alikuwa jijini Milan, the Gala del Calcio kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Italia .

Wakala wa Ronaldo, Jorge Mendes alipoulizwa kuhusu kukosekana kwa Ronaldo katika tuzo za Ballon D’or alitoa jibu hili .

“Cristiano Ronaldo ni mchezaji bora kuwahi kutokea na mnajua hilo,” amesema.

Mkurugenzi wa Michezo wa Juventus Fabio Paratici alimsifia Ronaldo katika hafla ya tuzo za Serie A kwa kusema kwamba Ronaldo alistahili kutwaa tuzo ya Ballon D’or .

Na aliongeza kwa kusema,” Mara zote huwa tunasema kwamba sifa za hizi tuzo ni mdahalo mkubwa”.