Msanii Jay Z atimiza miaka 50, kuachia albam zake mtandaoni

0
6

Nguli wa muziki wa Hip Hop duniani na Trilionea wa kwanza kwenye Hip Hop, rapa JAY-Z leo ametimiza miaka 50 ya kuzaliwa kwake.

Kuadhimisha siku hiyo, Jay-Z amerudisha album zake zote kwenye mtandao hasimu wa Spotify.

Kumbuka Jay Z ni mmiliki wa mtandao wa TIDAL ambao pia unafanya vizuri kwenye kusikiliza na kupakua muziki wa wasanii mtandaoni.

Jay-Z aliziondoa album hizo 9 kati ya 12 mwezi April mwaka 2017 na kufanya zipatikane Exclusively kwenye TIDAL.