Rais Trump amshambulia Macron – MUUNGWANA BLOG

0
8

Rais wa Marekani Donald Trump leo amemshambulia rais Emmanuel Macron kuhusiana na ukosoaji wa rais huyo wa Ufaransa kwa NATO na kuwakosoa mataifa mengine wanachama wa ushirika huo wa kijeshi kwa kuchukua hatua za taratibu mno kuongeza bajeti zao za ulinzi.

Wakati mawaziri wakuu na marais wa mataifa 29 wanachama wa ushirika huo wa kijeshi wakijikusanya mjini London kuadhimisha miaka 70 tangu kuasisiwa jumuiya hiyo.

Trump amewaambia waandishi habari kwamba matamshi ya Macron ni ya upuuzi, wakati alipolalamika kuwa NATO ni mahututi, kwa kuwa kwa sehemu kubwa ni juu ya ukosefu wa uongozi wa Marekani.

Macron alikasirika wakati Trump alipoyaondoa majeshi ya nchi yake kutoka kaskazini mwa Syria mwezi uliopita, hatua ambayo Uturuki iliona ni fursa ya kuvamia.

Uhusiano kati ya Marekani na Ufaransa umetetereka wiki hii baada ya mwakilishi wa biashara wa Marekani kupendekeza kuanzisha ushuru katika bidhaa za dola bilioni 2.4 kwa kulipiza kisasi dhidi ya kodi zilizowekwa na Ufarans katika makampuni makubwa ya teknolojia.